Taarifa ya Hamas imesisitiza kuwa muqawama hautanyamaza kimya madhali Israel inaendeleza uvamizi na jinai zake dhidi ya Wapalestina.
Hamas imeongeza kuwa: "Tunataka kuzidisha oparesheni kali dhidi ya utawala ghasibu, kuvuruga mahesabu ya utawala huo na kudumisha umoja ili kushajiisha na kuendeleza mapambano hadi kushindwa kikamilifu maghasibu na kusitisha jinai zao."
Vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni huko nyuma vilitangaza kuwa ripoti za awali ziliashiria oparesheni ya ufyatuaji risasi iliyofanywa katika eneo la Ariel katika Ukingo wa Magharibi na kupelekea kujeruhiwa mlowezi mmoja wa Kizayuni.
Vyombo hivyo vya habari pia vimetangaza kuwa mtu aliyetekeleza oparesheni hiyo karibu na kitongoji cha Ariel katika eneo la Salfit alikimbia kutoka eneo la tukio baada ya oparesheni hiyo.
Vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni vimetangaza kuwa, oparesheni ya kumsaka mtu aliyetekeleza oparesheni hiyo tayari imeanza na kwamba Israel imeongeza wanajeshi wake katika eneo hilo na wanazuia kuingia katika baadhi ya maeneo likiwemo eneo la Salfit.
Vyanzo vya habari vya Kiibrania vimeripoti kuwa, risasi 15 zilililenga gari la mlowezi huyo wa Kizayuni.
342/
Your Comment