Msemaji wa Hamas, Hazim Qassim ameongeza kuwa harakati hiyo inafanya kazi kwa kuwajibika kikamilifu na ipo jadi katika mazungumzo hayo.
Qassim ameashiria kushiriki katika mazungumzo hayo Adam Boehler, Mjumbe Maalumu wa Marekani anayehusika na suala la mateka na akasema: Tunatumai kwamba duru hii ya mazungumzo itazaa matunda ya maana kuelekea awamu ya pili ili kuandaa utangulizi wa kusitishwa mashambulizi ya Israel, kuondoka Wazayuni maghasibu Ukanda wa Gaza na kutekelezwa mapatano ya kubadilishana mateka.
Katika upande mwingine, Abdul Latif al Qanou afisa mwingine wa ngazi ya juu wa Hamas amesema kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel haujaheshimu makubaliano ya kusimamisha vita na hii ni kinyume na matakwa ya jamii ya kimataifa na juhudi za usuluhishi zenye lengo la kufanikisha utekelezaji wa makubaliano na kuhitimisha vita.
Afisa huyo wa Hamas amesema: Wanachosubiri sasa ni hatua mpya katika mazungumzo ya Doha kwa shabaha ya kutekeleza awamu ya pili ya makubaliano na kuruhusu misaada kuingia Gaza na kupatiwa hakikisho la kumalizika vita.
342/
Your Comment