Taasisi ya Kufuatilia Haki za Binadamu ya Euro- Mediterranean imeeleza katika ripoti yake ya karibuni kuwa Israel imewauwa Wapalestina 150 yaani katika kiwango cha wastani katika kila masaa 24 utawala huo umewauwa Wapalestina watatu.
Ripoti ya Euro-Med aidha imeeleza kuwa, tangu kuanza kwa makubaliano ya kusitisha mapigano, Israel pia imejeruhi Wapalestina 605 huko Gaza, yaani kiwango cha watu 11.8 kwa siku.
Utawala wa Israel umewalenga kikamilifu Wapalestina ambao nyumba zao ziko karibu na "eneo lililoanzishwa eti la usalama" kwenye mpaka wa kaskazini na mashariki mwa Gaza.
Taarifa ya Taasisi ya Kufuatilia Haki za Binadamu ya Euro- Mediterranean imeongeza kuwa: Sera za mauaji ya kimbari za utawala wa kizayuni zimeibua mazingira hatari ambayo yamesababishwa vifo vya pole pole vya Wapalestina.
Mzingiro haramu wa Israel dhidi ya Gaza umeliathiri pakubwa eneo hilo na hivyo kukwamisha kuingia misaada na huduma muhimu za kibinadamu kwa ajili ya wakazi wa ukanda huo.
Taasisi hiyo ya haki za binadamu pia imetahadharisha kuhusu kushtadi mgogoro wa kibinadamu iwapo mzingiro wa Israel utaendelea dhdi ya Gaza.
"Nchi na taasisi zote husika zinapasa kutimiza wajibu wao wa kisheria na kuchukua hatua za haraka kukomesha mauaji ya kimbari katika Ukanda wa Gaza", imeongeza taarifa ya taasisi hiyo ya kufuatilia haki za binadamu.
342/
Your Comment