15 Machi 2025 - 17:35
Karamu ya Iftar kwa watu 10,000 mahsusi kwa Mazuwwari wa Haram ya Imam Ridha (a.s) katika ua wa Imam Hassan al-Mujtaba (a.s.)

Kutokana na juhudi za Kitengo cha Maeneo Matukufu ya Madhabahu (Haram) Tukufu ya Razavi na katika mkesha wa kuzaliwa Ahlu al-Bayt (AS), Madhabahu Tukufu ya Razavi inawakaribisha mahujaji 10,000 waliofunga katika uwanja wa Imam Hassan Mojtabi (AS).

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahl al-Bayt (a.s) - Abna - Sambamba na Usiku wa Kumi na Tano wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, ambao unasadifiana na Siku ya kuzaliwa yenye baraka ya Mkarimu wa Ahl al-Bayt (a.s), Imam Hassan al-Mujtaba (a.s), Meza za iftar zilizoratibiwa kwa ukarimu wa Haram ya Imam Ridha (a.s) kama mwenyeji, ambapo (Haram hiyi) imewakaribisha Mazuwwari 10,000 na watu wanaofunga swaumu ya Ramadhani kwa ajili ya iftari katika ua wa Imam Hassan Al-Mujtaba (a.s).

Hafla hii ya Iftar itaanza saa 17:00 kwa usomaji wa Qur'an Tukufu, hotuba, utekelezaji wa programu maalum na sala za jamaa, kisha watumishi wa Razavi (Watumishi wa Haram ya Imam Reza amani iwe juu yake) watawakaribisha waumini waliofunga kwenye meza za Iftar.

Ukumbi wa Hazrat Zahra (S.A) pia utakaribisha watu 2,000 kwenye Meza za Iftar, kama vile ilivyokuwa katika nyusiku zilizopita.

Your Comment

You are replying to: .
captcha