15 Machi 2025 - 21:55
Source: Parstoday
UN: Hatua za kimataifa zichukuliwe dhidi ya ongezeko la 'chuki dhidi ya Waislamu'

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, ameelezea wasiwasi wake juu ya "ongezeko la chuki dhidi ya Waislamu", akitoa wito kwa serikali kulinda uhuru wa kidini, na kwa majukwaa ya mtandaoni kuzuia matamshi ya chuki.

Guterres ameyasema hayo leo Jumamosi katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupambana na Chuki dhidi ya Uislamu inayoadhimishwa kila mwaka Machi 15.

Mashirika ya kutetea haki za binadamu kote duniani na Umoja wa Mataifa kwa sasa yanapaza sauti dhidi ya ongezeko la chuki dhidi ya Uislamu na chuki dhidi ya Waarabu tangu baada ya kuanza vita vya miezi 17 vya Israel dhidi ya watu wa Ukanda wa Gaza huko Palestina.

“Tunashuhudia ongezeko la kutia wasiwasi la chuki dhidi ya Uislamu. Kuanzia kueneza wasifu wa kimbari na sera za kibaguzi zinazokiuka haki na utu wa binadamu, hadi unyanyasaji wa moja kwa moja dhidi ya watu binafsi na maeneo ya ibada,” amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika ujumbe wa video kwenye mtandao wa X. Ameongeza kuwa: “Hii ni sehemu ya janga kubwa la kutovumiliana, itikadi kali na mashambulizi dhidi ya makundi ya kidini na watu walio hatarini.”

UN: Hatua za kimataifa zichukuliwe dhidi ya ongezeko la 'chuki dhidi ya Waislamu'

Antonio Guterres ametoa wito kwa serikali, bila kutaja taifa lolote, "kukuza mshikamano wa kijamii na kulinda uhuru wa kidini".

Ameongeza kuwa: "Mitandao ya kijamii lazima izuie matamshi ya chuki na unyanyasaji. Na lazima sote tuzungumze dhidi ya ubaguzi wa rangi, chuki dhidi ya wageni na ubaguzi.” 

Wakati huo huo, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Miguel Angel Moratinos, amesema Waislamu wanakabiliwa na "ubaguzi wa kitaasisi na vikwazo vya kijamii na kiuchumi".

Angel Moratinos ameliambia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwamba: "Upendeleo kama huo unadhihirika katika unyanyapaa na mienendo ya ubaguzi wa rangi kwa Waislamu na inaimarishwa na vyombo vya habari vyenye upendeleo, matamshi na sera za chuki dhidi ya Uislamu za baadhi ya viongozi wa kisiasa." 

UN: Hatua za kimataifa zichukuliwe dhidi ya ongezeko la 'chuki dhidi ya Waislamu'

Katika wiki za hivi karibuni, waangalizi wa haki wamechapisha data inayobainisha viwango vya rekodi za matukio ya chuki dhidi ya Uislamu na matamshi ya chuki katika nchi kama vile Uingereza, Marekani na India.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha