16 Machi 2025 - 00:19
Ramadhani ni Fursa ya Wakati

"Kila Muislamu anapaswa kuamini kuwa: Kuwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni fursa ya wakati. Hivi ndivyo Mtume Muhammad (s.a.w.w) na Ahlul-Bayt wa Mtume (a.s) pamoja na Masahaba wema walivyokuwa wakiamini, kwao Ramadhani haukuwa ni Mwezi kama Miezi mingine".

Kwa Mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA -, Hojjatul Islam wal-Muslimin, Sheikh Reihan Yasin, ambaye pia ni Mwalimu wa Jamiatul-Mustafa Dar-es-Salam Tanzania, amesema katika moja ya darsa zake za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kuwa kila Muislamu anapaswa kuamini kuwa: Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni fursa ya wakati. Na hivi ndivyo Mtume Muhammad (s.a.w.w) na Ahlul-Bayt wa Mtume (a.s) pamoja na Masahaba wema walivyokuwa wakiamini, kwao Ramadhani haukuwa ni Mwezi kama Miezi mingine, bali ulikuwa ni Mwezi wenye nafasi  maalum katika nyoyo zao, na walidhihirisha hilo kupitia maandalizi yao kwa ajili ya Ramadhan, Furaha yao kwa ajili ya Ramadhan, na dua zao na ibada zao kwa wingi kwa ajili ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu.

Walikuwa wakifanya hivyo kwa sababu walijua fadhila, ukubwa wa hadhi ya Mwezi wa Ramadhan mbele ya Mwenyezi Mungu. Na walikuwa wakimuomba Mwenyezi Mungu awafikishe katika Mwezi wa Ramadhan wakiwa na swiha na afya njema ili waweze kufunga na kutekeleza ibada mbali mbali ndani yake.

Kwa hiyo, Dua ya kuomba kuwafikishwa kuifikia Ramadhani na kuwa na utayari wa kutosha kwa ajili ya Ramadhan, ni Sunna Tukufu ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w).

Ramadhani ni Fursa ya Wakati

Aidha, katika sehemu ya darsa lake amebainisha nukta muhimu anazotakiwa kujipamba nazo Muislamu katika Mwezi wa Ramadhani, ili aweze kuifunga Ramadhani kwa ukamilifu zaidi. Sifa hizo ni hizi zifuatazo:

  1. النية الخالصة :

إِنَّمَا اَلْأَعْمَالُ بِالنِّيَّاتِ وَ إِنَّمَا لِكُلِّ اِمْرِئٍ مَا نَوَى

"Matendo yanatokana na nia, na kila mtu atapata tu kile alichokusudia"

1-Kuwa na Nia safi:

Mfungaji anatakiwa kuwa na Nia safi ya kuazimia kumtii Mwenyezi Mungu, kuzidisha matendo mema na mazuri, na kuyahama maovu, na kuitumia vuzuri fursa ndani yake kwa ajili ya kuchuma radhi za Mwenyezi Mungu.

2. التوبة الصادقة:

2-Toba ya Kweli:

Toba ni wajibu kwa wakati wote na kwa kila dhambi. Lakini kwa wakati huu (unapokuwa kuingia ndani ya Ramadhan, ambao miongoni mwa sifa zake ni Mwezi wa Toba), Toba inakuwa ni wajibu zaidi, kwa nini?, ni kwa sababu unapoingia katika msimu kama huu wa utiifu (Twa'a), unategemea kumtii sana Mwenyezi Mungu ndani yake,  na unatarajia kujenga ukaribu na Mahusiano mazuri na Mwenyezi Mungu (s.w.t). Na hakuna shaka kwamba:

وصاحب المعصية لا يوفّق للطاعة ولا يؤهل للقرب

Na mtenda dhambi na maasi, hawezi kupata Taufiq ya kumtii Mwenyezi Mungu, na hawazi pia kuwa na maandalizi ya kujikurubisha karibu na Mwenyezi Mungu.

3. معرفة شرف الزمان

3- Kutambua thamani ya Wakati:

Wakati unayo thamani kubwa sana. Wakati ni maisha, na ni mtaji wako ambao unautumia kufanya biashara na Mwenyezi Mungu na kutafuta furaha na saada kupitia wakati, na kila sehemu ya wakati huu ambayo itapotea bure bila ya matendo mema, hilo litapelekea mja kukosa kuipata furaha saada ya duniani na akhera.

إذا كان رأس المال عمرك فاحترز عليه من الإنفاق في غير واجب

"Ikiwa mtaji wako ni Umri wako, basi kuwa mwangalifu usiutumie (kwenye mambo yasiyokuwa na umuhimu wowote)".

ساعةُ الذكر فاعلم أنه ثروةٌٌ وغنى، وساعةُ اللهو إفلاسٌ وفاقاتٌ

Muislamu anapaswa atambue kuwa:

"Saa moja tu ya kukaa na akafanya dhikri, ni utajiri na ni mali, na saa moja ya (kukaa kwake na kufanyaya upuuzi) ni kufilisika na ufukara bali ni umasikini".

Ramadhani ni Fursa ya Wakati

Mwenyezi Mtukufu wa Ramadhani ni Rabi'ul Qulub. Kwa maana: Ramadhani ni msimu wa mvua katika mioyo za Waumini. Kupitia Mwezi huu Mtukufu mja anapata fura ya kujenga ukaribu na Mola wake Mtukufu.

Ramadhani ni Fursa ya Wakati

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha