Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahl al-Bayt (AS) - Abna - Mawaziri wa Mambo ya nje wa Somalia na eneo linalojitenga "Somaliland" wametangaza katika masaa ya mwisho ya siku ya Ijumaa iliyopita kwamba hawajapokea ofa yoyote kutoka kwa Marekani au utawala wa Israel kwa ajili ya kuwapa makazi mapya Wapalestina wa Gaza. Wakati huo huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Somalia alikataa vikali jaribio lolote lile na hatua yoyote ile kwa lengo hili.
Hapo awali, Shirika la Habari la "Associated Press", likiwanukuu maafisa wa Marekani na Israel, liliripoti kwamba Serikali ya Marekani na Serikali ya Israel iliwasiliana na maafisa kutoka Sudan, Somalia, na eneo linalojiendesha la Somaliland ili kujadili matumizi ya eneo lao kwa ajili ya kuwapatia makazi mapya Wapalestina wa Gaza.
Kulingana na ripoti ya Associated Press, mamlaka za Sudan zimesisitiza kwamba zinakataa pendekezo lolote la Marekani katika suala hili; Maafisa wa Somali na Somaliland pia walibainisha kuwa hawakujua na hawajui mawasiliano yoyote kama hayo.
"Ahmed Moallim Fiqi Ahmed", Waziri wa Mambo ya Nje wa Somalia, alisema kuwa nchi yake "inakataa kwa uthabiti pendekezo au mpango wowote wa chama chochote ambacho kinakiuka haki ya watu wa Palestina kuishi katika ardhi ya mababu zao." Aliiambia Reuters kwamba Serikali ya Somalia haijapokea mapendekezo yoyote kuhusu suala hili, akiongeza kuwa Mogadishu inapinga mipango yoyote ya kutumia eneo la Somalia ili kuwapa makazi watu wa taifa lingine.
Abd al-Rahman Zahir, Waziri wa Mambo ya Nje wa Mkoa unaojiendesha wa Somaliland, pia alisema "Hakuna mazungumzo na upande wowote kuhusu Wapalestina."
Your Comment