New York Times limetathmini kuwa oparesheni za kijeshi za Marekani dhdi ya harakati ya Ansarullah ya Yemen haziwezi kuisambaratisha harakati hiyo na kutoa pigo kwa Wayemen na hivyo kuondoa tishio kwa meli zenye mfungamano na utawala wa kizayuni wa Israel katika Bahari Nyekundu.
Gazeti la New York Times limeandika kuwa: Wachambuzi wa masuala ya Asia Magharibi waliohojiwa na gazeti hilo wanaamini kuwa wanamapambano wa harakati ya Ansarullah ambao gazeti hilo limewataja kuwa ni wanamapambano wa Ansarullah ya Yemen, wamedhihirisha uwezo wao wa kuendesha mapambano mkabala wa nguvu za kijeshi zinazoonekana kuwa bora zaidi yaani Marekani; na kama wanavyodai wanasisasa wa Kimagharibi wanamapamano hao hawaitegemei Iran.
New York Times limeendelea kuandika: Jack Kennedy, mkuu wa kitengo cha Masuala ya Dharura cha Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika katika kampuni ya S&P Global Market Intelligence amesema: "Operesheni moja ya kijeshi, hasa operesheni ya mashambulizi ya anga, haitoshi kutoa pigo la kudumu kwa wapiganaji wa Ansarullah wa Yemen na kusimamisha kabisa mashambulizi yao.
Gazeti la The New York Times limeandika: Makampuni makubwa zaidi ya meli duniani yameepuka kupitisha meli zao katika Bahari Nyekundu na sasa yamelazimika kutumia njia ya muda mrefu kuzunguka bara la Afrika wakihofia mashambulizi ya harakati ya Ansarullah kufuatia kuongezeka kwa mivutano huko Asia Magharibi kulikosababishwa na mashambulizi na vita vya Israel dhidi ya Gaza mwezi Oktoba mwaka 2023.
Wanamapambano wa Ansarullah wamekuwa wakizishambulia meli zinazoelekea Israel katika Bahari Nyekundu ili kuwaunga mkono wananchi wa Palestina dhidi ya mashambulizi ya Israel huko Gaza.
342/
Your Comment