22 Machi 2025 - 21:33
Source: Parstoday
UN: Vifo vya wahamiaji vilivunja rekodi mwaka jana, karibu 9,000 wamekufa

Takwimu mpya zilizotolewa na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) zinaonyesha kuwa, karibu watu 9,000 walikufa mwaka jana wakijaribu kuvuka mipaka.

Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) limerekodi vifo vya wahamiaji wasiopungua 8,938 mwaka 2024, na kuweka rekodi mpya kwa mwaka wa tano mfululizo.

Hata hivyo, shirika hilo linasema idadi halisi ya vifo vya wahamiaji huenda ni kubwa zaidi ikizingatiwa kwamba vifo vingi haviripotiwi au kuthibitishwa.

Taarifa iliyotolewa na Mratibu wa Miradi ya Wahamiaji Waliopotea wa IOM, Julia Black, imesema: "Ongezeko la vifo ni la kuogofya, lakini ukweli kwamba maelfu ya watu wanaendelea kutotambuliwa kila mwaka ni maafa makubwa zaidi." 

Bara la Asia limeongoza kwa watu walipoteza maisha wakijaribu kuvuka mipaka, likifuatiwa na Afrika na Ulaya. Watu 2,452 waliripotiwa kupoteza maisha baada ya boti walizokuwa wakisafiria kuelekeka barani Ulaya, kuzama katika Bahari ya Mediterenian.

UN: Vifo vya wahamiaji vilivunja rekodi mwaka jana, karibu 9,000 wamekufa

Ukanda wa Bahari ya Atlantiki kati ya Afrika Magharibi na Visiwa vya Kanari vya Uhispania pia ni mojawapo ya njia mbaya zaidi za uhamiaji duniani.

Karibu watu 47,000 ambao walivuka mwaka jana walifika visiwa hivyo, na kuvunja rekodi za hapo awali kwa mara ya pili.

Wengi wao walikuwa raia wa Mali, Senegal na Morocco, na wengi walipanda boti za kuelekea Uhispania kutoka pwani ya Mauritania.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha