Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza sera ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kunyoosha mkono wa udugu kwa madola yote ya Kiislamu na kusema: Njia ya kukabiliana ipasavyo na jinai zisizo na kifani za utawala wa Kizayuni (Israel) na waungaji mkono wake huko Palestina na Lebanon ni umoja, mshikamani na ushirikiano kati ya nchi zote za Kiislamu.
Katika kikao hicho, Imam Khamenei ameupongeza Umma wa Kiislamu na taifa la Iran kwa kusherehekea sikukuu iliyobarikiwa ya Idul Fitr, akiitaja kuwa ni miongoni mwa mambo yanayoukutanisha pamoja Ulimwengu wa Kiislamu na kuzidisha adhama ya Uislamu na Mtume Muhammad (saw). Ameongeza kuwa: Sharti la kuongezeka heshima ya Uislamu ni umoja, azma na utambuzi wa Umma wa Kiislamu.
Akizungumzia matukio ya kimataifa yanayojiri kwa haraka na kufuatana, Ayatullah Khamenei amesema: "Katika kukabiliana na matukio hayo yenye kasi kubwa, nchi za Kiislamu lazima zibainishe haraka na kwa usahihi misimamo yao, kufikiria na kuweka mipango."
Amesisitiza kwamba Umma mzima wa Kiislamu ni familia moja na serikali za nchi za Waislamu lazima zifikiri na kutenda kwa mujibu wa mtazamo huo. Ameongeza kuwa: "Jamhuri ya Kiislamu inanyoosha mkono wake kwa serikali zote za nchi za Kiislamu na inajiona kuwa ni ndugu yao."
Vilevile amezungumzia kujeruhiwa Palestina na Lebanon kutokana na jinai ziinazofanywa na utawala wa Kizayuni na waungaji mkono wake, na kusisitiza ulazima wa Ulimwengu wa Kiislamu kusimama kidete kukabiliana na mateso hayo. Amesema: "Umoja, uelewa na mshikamano wa nchi za Kiislamu, unazifanya pande nyingine kutafakari juu ya vitendo vyao, na tunatumai kuwa viongozi wa nchi za Kiislamu wataweza kuunda Umma wa Kiislamu kwa maana yake halisi kwa hamasa na harakati zao za kweli"
342/
Your Comment