31 Machi 2025 - 22:07
Source: Parstoday
Utawala wa Kizayuni waendelea kupinga utoaji wa misaada kwa Wapalestina

Vitendo vya kikatili vya utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina wanaoishi Gaza vinaendelea, na bado utawala huo unazuia kufikishwa kwa misaada ya chakula na dawa kwa wakazi wa Gaza.

Katika muktadha huo, Tom Fletcher, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya kibinadamu na uratibu wa misaada ya dharura, amesema: "Kwa sababu ya upinzani wa Israel, misaada ya chakula inaoza katika mipaka ya Gaza."

Akitaja kuwa misaada ya chakula iko kwenye hatari ya kuoza mipakani na dawa kuisha, amesema: "Hata hawaruhusu uingizaji wa vifaa muhimu vya matibabu."

Naibu Katibu Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amekosoa kutochukua hatua kwa jamii ya kimataifa dhidi ya uhalifu huo, akisema: "Iwapo misingi ya sheria za kibinadamu bado inaheshimiwa, basi jamii ya kimataifa inapaswa kuchukua hatua kuilinda."

Kwa kuendelea kwa mashambulizi ya utawala wa Kizayuni wa Israel baada ya utawala huo katili kuvunja mapatano ya usitishaji wa vita, hali huko Gaza imekuwa ya hatari mno. Utawala huo dhalimu umeongeza mashinikizo dhidi ya Wapalestina kwa njia mbalimbali za kisiasa na kijamii, ikiwa ni pamoja na kuzuia kuingia kwa chakula na dawa. Kuhusiana na hili, Ismail Thawabteh, Mkurugenzi wa Ofisi ya Habari ya Serikali ya Palestina huko Gaza, hivi karibuni alitangaza kuwa: "Utawala wa Kizayuni bado umeweka mzingiro mkali dhidi ya Gaza na tangu mwanzo wa mwezi wa Ramadhani, umefunga kabisa mipaka yote ya eneo hilo. Israel imezuia zaidi ya malori 10,000 ya misaada ya kibinadamu yamezuiwa kuingia Gaza – jambo ambalo ni uhalifu wa kuwanyima watu wa Palestina chakula kwa makusudi."

Hali hii inatokea huku takwimu kutoka Gaza zikionyesha kuwa zaidi ya watoto 3,500 wamekumbwa na vifo kutokana na utapiamlo, zaidi ya wagonjwa 350,000 wenye maradhi maalumu wanahitaji dawa, magonjwa ya kuambukiza yanaendelea kuenea, na ukosefu wa chakula ni wa wazi kabisa.

Kwa kweli, utawala wa Kizayuni unaendeleza mauaji ya Wapalestina kwa njia mbalimbali, ikiwemo kuzuia misaada – hali ambayo ni uvunjaji wa wazi wa sheria za kimataifa za kibinadamu. Lakini licha ya sera na uhalifu huu, nchi za Magharibi zinayapuuza yaliyopo Gaza na hazichukui hatua yoyote kulingana na madai yao ya kutetea haki binadamu.

Utawala wa Kizayuni waendelea kupinga utoaji wa misaada kwa Wapalestina

Katika hili, Marekani kama kinara wa nchi za Magharibi haijakaa kimya tu kuhusu sera za  utawala Israel dhidi ya Wapalestina, bali pia imeendelea kuusaidia utawala huo katili kwa misaada ya kijeshi na kisiasa, jambo ambalo limempa Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa Israel, kiburi zaidi kuendelea na mauaji dhidi ya wakazi wa Gaza bila kujali sheria za kimataifa.

Kuhusiana na hilo, Abu Ubaida, msemaji wa tawi la kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, alisema: "Watu wa Palestina wanakabiliwa na mauaji ya halaiki na njaa huku dunia ikiwa mtazamaji."

Kwa hivyo, Israel ambayo ilipata pigo kubwa licha ya uhalifu wake katika vita vya Gaza, sasa inajaribu kwa njia nyingine kuendeleza sera ya mauaji ya Wapalestina na kuwakandamiza – ambapo kufunga njia za kuingiza misaada ni sehemu ya mkakati huo. Viongozi watenda jinai wa Kizayuni ambao wameweka lengo la kuwalazimisha Wapalestina kuhama, wanajaribu kutumia sera mbalimbali ili kuwafanya wakaazi wa Gaza kuondoka au kufa polepole kwa njaa. Kituo cha Uangalizi wa Haki za Binadamu cha Ulaya-Mediterrania kimetangaza kuwa: "Utawala wa Kizayuni hautumii misaada ya kibinadamu tu kama chombo cha mashinikizo katika mazungumzo ya kisiasa au kijeshi, bali unatekeleza kwa makusudi na kwa mpangilio sera ya kuwanyima Wapalestina chakula, ili hali ya maisha kuwa mbaya iwashinikize wakaazi wa Gaza kuondoka."

Licha ya hali mbaya sana, Wapalestina wa Gaza wanaendelea na maisha na mapambano yao, kama viongozi wa Hamas walivyosisitiza mara kwa mara. Hazem Qassem, msemaji wa harakati ya Hamas, amesema: "Tunatoa onyo kwa wavamizi kuhusu kuendelea kwa uhalifu huu, na tunasisitiza kuwa watu wa Palestina wataendeleza mapambano na hawatasalimu amri mbele ya mashinikizo, na wataendelea kusimama imara hadi wapate uhuru na ushindi."

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha