31 Machi 2025 - 22:09
Source: Parstoday
Kiongozi mwandamizi wa HAMAS: Muqawama na Silaha zake, kwetu sisi ni mstari mwekundu

Bassem Naim, kiongozi mwandamizi wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema: "kwetu sisi tukiwa ni taifa linalokaliwa kwa mabavu, Muqawama na silaha zake ni mstari mwekundu na ni suala la uwepo wetu na uhai wetu".

Naeem ameongezea kwa kusema: "Harakati ya Hamas inaendelea kuheshimu makubaliano yaliyotiwa saini Januari 19, 2025.

Kiongozi huyo mwandamizi wa Hamas amebainisha kuwa, pendekezo jipya ambalo Muqawama umeliwasilisha kwa wapatanishi ni jitihada za kuivuka hali mbaya na ya mgogoro iliyopo.Kuanzia Oktoba 7, 2023 hadi Januari 19, 2025 utawala wa Kizayuni wa Israel kwa uungaji mkono kamili wa Marekani ulikuwa ukiendesha vita angamizi dhidi ya wakazi wa Ukanda wa Ghaza ambavyo vimesababisha uharibifu mkubwa na maafa makubwa ya roho za watu, hata hivyo haujaweza kufikia malengo yake yaliyotajwa ya kuiangamiza harakati ya Hamas na kuwakomboa mateka wa Kizayuni.

Hatimaye mnamo Januari 19, 2025 usitishaji vita ulitekelezwa katika Ukanda wa Ghaza kulingana na mpango uliopendekezwa na serikali ya Marekani na kuafikiwa na pande mbili za utawala wa Kizayuni na harakati ya Hamas.Hata hivyo, mnamo Machi 18 utawala ghasibu wa Israel ulianzisha tena mashambulio yake ya kinyama ya kijeshi dhidi ya Ghaza kinyume na masharti ya usitishaji vita, hatua ambayo imelaaniwa vikali kimataifa.

Mashambulio hayo hadi sasa yameua shahidi Wapalestina wasiopungua 921 na kuwajeruhi wengine 2,054.Kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Palestina katika Ukanda wa Ghaza idadi ya Wapalestina waliouawa shahidi katika eneo hilo tangu ilipotekelezwa Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa Oktoba 7, 2023 hadi sasa imefikia watu 50,277 na idadi ya waliojeruhiwa imefikia 114,095.../

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha