Chaneli ya 12 ya televisheni ya Israel imeripoti kuwa licha ya kuongezeka mashambulizi ya Marekani dhidi ya Yemen, mashambulizi hayo hayajawa na athari yoyote na inavyoonyesha, hayajaweza kupunguza au kusimamisha kiwango cha makombora yanayorushwa kuelekea Israel.
Televisheni hiyo ya utawala wa Kizayuni imekiri kwamba kombora la Yemen lililorushwa kuelekea ardhi zinazokaliwa kwa mabavu siku ya Jumapili lilipelekea mamilioni ya Wazayuni kukimbilia kwenye mahandaki yao ya maficho.Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Kizayuni, watu kadhaa wamejeruhiwa kutokana na taharuki iliyozuka na pupa ya kukimbilia mafichoni katika ardhi hizo za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu zilizopachikwa jina bandia la Israel.
Brigedia Jenerali Yahya Saree, msemaji wa Vikosi vya Ulinzi vya Yemen, alitangaza katika taarifa jana Jumapili kwamba kombora la balestiki la Zulfiqar lililorushwa kuelekea Uwanja wa Ndege wa Ben Gurion huko Jaffa (Tel Aviv) lililenga kwa mafanikio shabaha iliyokusudiwa. Aidha, Saree ametangaza kuwa katika muda wa saa 24 zilizopita, vikosi vya ulinzi vya nchi hiyo vimepambana mara tatu na manowari ya kubebea ndege za kivita ya Marekani ya Truman na manowari nyingine za kivita katika eneo la Bahari Nyekundu.
Msemaji wa Vikosi vya Ulinzi vya Yemen ameendelea kusema: "kwa kutekeleza operesheni hii, tumeonyesha kuwa, Marekani imeshindwa kuizuia Yemen isiwasaidie na kuwaunga mkono wananchi wanaodhulumiwa wa Palestina; na mashambulizi ya anga ya Marekani hayatuzuii sisi kutekeleza majukumu yetu ya kidini, kimaadili na kiutu. Kwa msaada wa Mwenyezi Mungu, tutaendeleza operesheni dhidi ya Wazayuni hadi uvamizi na mzingiro dhidi ya Ukanda wa Ghaza utakaposimamishwa".../
342/
Your Comment