Vyombo vya habari vya Palestina vimetangaza kuwa, watu 15 wameuliwa shahidi katika mshambulizi ya ndege za kivita za utawala wa Kizayuni dhidi ya nyumba moja ya makazi ya raia katika mtaa wa al Mansurah katika eneo la Shujaiya katika mji wa Gaza. Ripoti zinasema kuwa watu kadhaa waliouliwa shahidi katika hujuma hiyo ya Israel wangali chini ya vifusi.
Katika upande mwingine, jeshi la Israel limeshambulia vikali kwa mizinga eneo la kusini mwa Ukanda wa Gaza. Katika hujuma hiyo ya kinyama, jeshi la Israel limeteketeza nyumba nyingine iliyokuwa makazi ya raia wa Kipalestina katika eneo la Qizan al-Najjar, kusini mwa mji wa Khan Yunis kusini mwa Gaza na kumuuwa shahidi raia mmoja.
Duru za habari za Palestina zimetangaza kuwa Wapalestina wasiopungua 24 wameuawa shahidi katika mashamulizi ya anga ya Israel dhidi ya Gaza mapema leo asubuhi.
Jeshi la Israel pia limelishambulia eneo la Tel al Sultan huko magharibi mwa mji wa Rafah pia ambapo vifaru vya utawala huo haramu vimeripotiwa vikitekeleza mashambulizi pia katika eneo hilo.
342/
Your Comment