Saudi Arabia, Umoja wa Falme za Kiarabu, Qatar na Kuwait zimeeleza kutiwa wasiwasi na matamshi ya karibuni ya kushupalia vita ya Rais wa Marekani Donald Trump dhidi ya Iran, ambapo alitishia "kuishambulia Iran kwa mabomu kwa namna ambayo wao (Wairani) hawajawahi kuona hapo awali."
Gazeti la Middle East Eye likinukuu 'afisa wa ngazi ya juu' wa Marekani limeripoti kuwa, idadi ya safari za ndege za kijeshi za Marekani katika eneo hili zimeongezeka kwa asilimia 50, ikilinganishwa na safari hizo huko nyuma.
Katika kukabiliana na marufuku ya mataifa ya Ghuba ya Uajemi, Marekani imekusanya ndege za B-2 zilizotumiwa katika mashambulizi ya hivi majuzi dhidi ya Yemen katika kambi ya Diego Garcia katika Bahari ya Hindi.
Wiki iliyopita, Harakati ya Ansarullah ya Yemen ilionya kuwa itashambulia Abu Dhabi na Dubai ikiwa "vitendo vya kizembe" vya Imarati kupitia ushirikiano na Marekani katika mashambulizi dhidi ya Yemen vitaendelea. Trump alisema siku ya Jumatatu kwamba, anapanga kuzuru Saudi Arabia na mataifa mengine ya Ghuba ya Uajemi kufikia mwezi ujao wa Mei.
Wakati huo huo, Amir wa Kuwait, Nawaf Al-Ahmad Al-Jaber Al-Sabah katika mazungumzo ya simu na Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian jana JUmatano alisema kuwa, nchi yake kamwe haitaruhusu kitendo chochote cha uchokozi na hujuma kuanzishwa kutoka katika ardhi yake dhidi ya nchi nyingine.
342/
Your Comment