Wizara ya Afya mjini Sanaa imesema mashambulizi ya kikatili Marekani yamesababisha vifo vya raia 61 na kuwajeruhi wengine 139 tangu Machi 15 mpaka sasa.
Jeshi la Marekani limekuwa likifanya mashambulizi ya karibu kila siku nchini Yemen huku Rais Donald Trump akiahidi "kuwaangamiza kabisa" wanaharakati wa Ansarullah (Houthi).
Hata hivyo kundi hilo la Muqawama la Yemen limesema litaendelea na operesheni zake za kijeshi dhidi ya Israel na njia za meli katika Bahari Nyekundu hadi pale Israel itakapokomesha mashambulizi yake ya umwagaji damu dhidi ya Gaza, ambayo wataalamu wa Umoja wa Mataifa wameyataja kuwa mauaji ya halaiki.
Jeshi la Yemen limetangaza kuhusika na mfululizo wa mashambulizi hayo yaliyofanywa kwa ustadi wa hali ya juu na kuzipiga meli za kivita za Marekani, ikiwa ni pamoja na manowari ya USS Harry S. Truman ya kubebea ndege katika Bahari Nyekundu.
Opereshenei hizo za kishujaa za vikosi vya ulinzi vya Yemen zimefanywa kwa nia ya kuendelea kukabiliana na uvamizi wa Marekani dhidi ya Yemen; na pia kuliunga mkono taifa madhlumu la Palestina.
342/
Your Comment