9 Aprili 2025 - 21:20
Source: IQNA
Utawala wa Israel wafunga Msikiti wa Ibrahimi, mkurugenzi apigwa marufuku

Mamlaka ya utawala wa Kizayuni iliweka kufuli katika milango ya Msikiti wa Ibrahimi ulioko katika mji wa Al-Khalil (Hebron), kusini mwa Ukingo wa Magharibi, siku ya Jumatatu.

Aidha, walimkamata mmoja wa wafanyakazi wa msikiti huo, wakampiga marufuku mwingine, na kumuita mkurugenzi wa msikiti kwa mahojiano.

Sheikh Jamal Abu Aram, Mkurugenzi wa Waqfu wa Al-Khalil, aliiambia Ma’an News kuwa mamlaka za Kizayuni ziliamuru Sheikh Mutaz Abu Sneineh, mkurugenzi wa msikiti huo, kufika kwa ajili ya mahojiano baada ya kuchapisha picha zinazoonyesha kufuli zilizowekwa kwenye milango ya Msikiti wa Ibrahimi.

Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kidini ya Palestina imelaani hatua hiyo na kusema maeneo yote ya msikiti—vikiwemo vyumba vya makaburi na njia zake—ni miliki ya Idara ya Wakfu ya Kiislamu, ambayo ina haki ya kisheria ya kushikilia funguo zake, na ikalaani hatua ya kufunga milango hiyo kama “shambulio la wazi na la kutisha dhidi ya heshima ya maeneo haya matakatifu.”

Kizuizi hiki kinakuja kufuatia hatua ya utawala wa Israel kukataa katika mwezi uliopita wa Ramadhani kufungua sehemu zote za msikiti kwa waumini, hata katika matukio muhimu kama vile Idul Fitr, Laylat al-Qadr na Ijumaa, kinyume na ilivyozoleleka.

Tangu mwaka 1994, baada ya mlowezi mmoja wa Kizayuni kuwafaytulia risasi na kuwaua Wapalestina 29 waliokuwa wakiswali katika Msikiti wa Ibrahimi, utawala wa Israel uliugawa msikiti huo, ambapo asilimia 63—ikiwemo chumba cha adhana—ilitengwa kwa ajili ya Wayahudi, huku asilimia 37 ikibaki kwa Waislamu.

Msikiti huo unaendelea kuwa chini ya udhibiti wa Israel, huku takribani wakoloni 400 wa Kiyahudi wakiishi katika Mji Mkongwe wa al-Khalil, wakiwa wanalindwa na askari wa Israel wapatao 1,500.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha