13 Aprili 2025 - 22:32
Source: Parstoday
Iran yaitaka UN kutumia uwezo wake kusitisha mauaji ya kimbari Ukanda wa Gaza

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameuhimiza Umoja wa Mataifa kutumia uwezo wake wote kusimamisha mauaji ya kimbari yanayofanywa na Israel katika Ukanda wa Gaza na mashambulizi yake dhidi ya watu wa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Saeed Khatibzadeh ameeleza haya leo katika mazungumzo yake na Rosemary Anne DiCarlo, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya kisiasa na amani. Mazungumzo hayo yamefanywa pambizoni mwa Kongamano la Nne la Diplomasia la Antalya nchini Uturuki lililofanyika kuanzia Aprili 11 hadi 13. 

Pande mbili zimejadili matukio muhimu ya kieneo na kimataifa, na kuangazia ukatili wa utawala ghasibu wa Israel dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Iran yaitaka UN kutumia uwezo wake kusitisha mauaji ya kimbari Ukanda wa Gaza

Khatibzadeh na DiCarlo

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amemuomba Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kutumia uwezo wote wa taasisi hiyo ya kimataifa kusitisha mauaji ya kimbari na pia mashambulizi dhidi ya Ukingo wa Magharibi wa mto Jordan.

Kwa upande wake, Bi DiCarlo amesema kuwa Umoja wa Mataifa tayari umechukua baadhi ya hatua kwa ajili ya kusimamisha vita na mauaji ya kimbari ya Israel na ameahidi kuchukua hatua zaidi katika uwanja huo. 

Khatibzadeh na DiCarlo pia wamejadili mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja yaliyofanywa jana na Iran na Marekani nchi mwenyeji ikiwa ni Oman.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha