Harakati hiyo imeongeza katika taarifa yake kwamba uhalifu huu unathibitisha kwamba utawala vamizi wa Israel unafanya kazi kwa baraka na kwa kushirikiana na Marekani, katika kivuli cha kusitishwa kikamilifu taasisi zote za kimataifa za kufuatia uhalifu kama huo.
Harakati hiyo imeibebesha Marekani dhima kamili ya uhalifu huo katika Hospitali ya Baptist, na kuongeza kwamba jinai hiyo isingefanyika bila taa ya kijani ya serikali ya Washington.
Hamas imetoa wito kwa jamii ya kimataifa, Umoja wa Mataifa na nchi za Kiarabu na Kiislamu kuchukua hatua za haraka kukomesha ukiukwaji huo wa wazi wa sheria za kimataifa.
Ripoti zinasema kwamba huduma katika Hospitali ya Baptist katika Jiji la Gaza zilisimama kikamilifu baada ya mashambulizi ya Israeli mapema leo Jumapili, huku wagonjwa na majeruhi waliokuwa wamelazwa hospitalini hapo wakilazimika kilala mitaani.
Televisheni ya al Jazeera ya Qatar imeripoti kuwa, jeshi la Israel limeshambulia hospitali hiyo kwa makombora mawili mapema leo na kusababisha uharibifu mkubwa.
Hujuma ya Isarel dhidi ya hospitali hiyo imefanyika sambamba na mashambulizi ya anga yanayoendelea kufanywa na utawala huo katika maeneo mbalimbali ya Ukanda wa Gaza.
342/
Your Comment