13 Aprili 2025 - 22:40
Source: Parstoday
Watetezi wa haki za binadamu wa Marekani wafungua kesi kusitisha vikwazo vya Trump dhidi ya maafisa wa ICC

Watetezi wa haki za binadamu wa Marekani wamewasilisha kesi mahakamani ili kusimamisha amri ya utendaji ya Rais Donald Trump ya kumwekea vikwazo Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), wakisema inakiuka vipengengee vya katiba kuhusu haki zao za uhuru wa kujieleza.

Kesi hiyo, iliyofunguliwa siku ya Ijumaa na mawakili wawili wanaowakilisha Muungano wa Uhuru wa Kiraia wa Marekani (ACLU), inasema kuwa vikwazo hivyo vinakiuka haki zao za kikatiba kwa kuzuia uwezo wao wa kuwasiliana na kushirikiana na ICC.

ICC iliyofunguliwa mwaka wa 2002, ni mahakama ya kudumu ya Umoja wa Mataifa yenye makao yake huko The Hague, na ina mamlaka ya kimataifa ya kufungua mashtaka ya mauaji ya kimbari, uhalifu dhidi ya ubinadamu na jinai za kivita katika nchi wanachama au ikiwa hali hiyo itaripotiwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Februari  mwaka huu Rais Donald Trump wa Marekani alitoa agizo lililoidhinisha vikwazo vikubwa vya kiuchumi na usafiri kwa watu wanaofanya kazi katika uchunguzi wa mahakama ya ICC dhidi ya raia wa Marekani au washirika wa Marekani kama vile Israel, akikariri hatua aliyochukua katika muhula wake wa kwanza wa urais.

Trump alichukua hatua hiyo baada ya mahakama hiyo ya kimataifa kutoa hati za kukamatwa waziri mkuu wa utawala wa Israel, Benjamin Netanyahu na waziri wa zamani wa vita wa utawala huo Yoav Gallant kwa kuhusika na vita vya mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina huko Gaza. 

Maelfu ya raia wa Palestina wanaendelea kuuawa na wengine zaidi ya milioni moja wamelazimishwa kuhama makazi yao kutokana na vita hivyo vya mauaji ya kimbari vya Israel.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha