14 Aprili 2025 - 19:53
Source: Parstoday
Kazem Gharib Abadi: Rafael Grossi kuwasili Tehran Jumatano

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Anayehusika na Masuala ya Kisheria na Kimataifa ametangaza kuwa, Rafael Grossi Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atiomiki (IAEA) atawasili Tehran Jumatano wiki hii na atakuwa na mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Mkuu wa Taasisi ya Nishati ya Nyuklia ya Iran.

Kazem Gharib Abadi ameongeza kuwa: Ziara hii inafanyika katika fremu ya kuendeleza maelewano na ushirikiano kati ya pande mbili. 

Kabla ya taarifa hii, Muhammad Eslami, Mkuu wa Taasisi ya Nishati ya Nyuklia ya Iran alisema wakati akijibu swali kuhusu mambo yatakayojadiliwa katika ziara tarajiwa ya Mkurugenzi Mkuu wa IAEA hapa nchini kwamba, kuna maeneo mawili. Sehemu ya kwanza ni kuhusu uhusiano wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na wakala wa IAEA, na sehemu ya pili inahusiana na Mkurugenzi Mkuu wa wakala huo. "Uhusiano wetu na IAEA umefafanuliwa kwa kuzingatia kanuni na Mkataba wa NPT;  Na katika mfumo wa vigezo vya kiufundi na kisheria, tuna mfumo mahususi wa ufuatiliaji ndani ya ambao lazima tuuwezeshe, na unatekelezwa na IAEA kulingana na mpango na ratiba maalumu.

Kazem Gharib Abadi: Rafael Grossi kuwasili Tehran Jumatano

Eslami ameongeza kuwa: "Hatuna tatizo lolote na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki. Mahusiano yetu ni ya kawaida kabisa na kwa mujibu wa mfumo wa kisheria. Lakini jambo linalotafakarisha ni kujihusisha Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo katika mijadala ya kisiasa. Siku zote tumekuwa tukisisitiza na tunakariri tena kwamba Mkurugenzi Mkuu wa IAEA hapasi kujiingiza katika masuala ya kisiasa, kwani suala hili lipo nje ya majukumu yake ya kiufundi na kisheria."

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha