Maria Zakharova amesema Moscow imejiandaa kwa ajili ya mazungumzo kati ya ujumbe wa kidplomasia wa Iran na Sergei Lavrov, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Russia.
"Tunasubiri kwa hamu wenzetu wa Iran. Tayari tumepanga ratiba kwa ajili ya mazungumzo ya ujumbe wa Iran na Waziri wa Mashauri ya Kigeni na viongozi wengine wa Russia", amesema Zakharova.
Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Russia ameeleza haya baada ya mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati ya Iran na Marekani nchini Oman. Mazungumzo yalifanyika siku ya Jumamosi kwa kuhudhuriwa na Steve Witkoff, Mjumbe Maalumu wa Rais Donald Trump wa Marekani na Abbas Araqchi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran na ujumbe aliofuatana nao.
Hii ni mara ya kwanza kufanyika mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati ya Iran na Marekani katika ngazi ya juu baada ya Trump kuiondoa Marekani kwa upande mmoja na kinyume cha sheria, katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA wakati wa muhula wake wa kwanza wa urais mwaka 2018.
342/
Your Comment