19 Aprili 2025 - 20:42
Source: Parstoday
Iran yataka kusitishwa kimya cha jamii ya kimataifa mkabala wa mashambulizi ya Marekani huko Yemen

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu iko bega kwa bega na wananchi wanamapambano wa Yemen na ametoa wito wa kukomeshwa kimya cha jamii ya kimataifa mbele ya ukiukwaji wa wazi wa sheria za kibinadamu na kanuni za kimataifa unaofanywa na Marekani dhidi ya watu wa Yemen.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameeleza haya katika radiamali yake kwa shambulizi la kinyama la anga la Marekani katika bandari ya Ras- Isa huko Yemen. 

Esmail Baqaei amelaani shambulio hilo lililofanywa na Marekani katika bandari ya Ras- Isa huko Yemen na kuuwa shahidi na kujeruhi makumi ya raia wasio na hatia na kuharibu miundombinu ya bandari hiyo. 

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameyataja mashambulizi hayo ya Marekani dhidi ya Yemen kuwa ni mfano wa wazi wa jinai na uhalifu, na ukiukaji mkubwa wa kanuni na sheria za kimsingi za Mkataba wa Umoja wa Mataifa na sheria za kimataifa.

Amesisitiza kuwa: Hujuma za Marekani dhidi ya Yemen zinafanyika katika fremu ya uungaji mkono wa pande zote wa nchi hiyo kwa Wazayuni maghasibu na mauaji yao ya kimbari dhidi ya Wapalestina, na imeifanya Marekani kuwa mshirika katika jinai na uhalifu wa Israel huko Palestina. 

Baqaei ametahadharisha kuwa: Kuendelea hujuma za kijeshi za Marekani dhidi ya watu wa Yemen, kuharibiwa miundombinu muhimu ya nchi hiyo na kuuawa Waislamu wa Yemen si tu kwamba kunauhamasisha utawala wa Kizayuni wa Israel kuendeleza jinai zake dhidi ya watu wa Palestina katika Ukanda wa Gaza na katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, bali pia ni sababu ya kushadidi ukosefu wa usalama katika eneo hili na kutishia amani na usalama wa kimataifa.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha