3 Mei 2025 - 23:18
Source: Parstoday
Khatibu wa msikiti wa al-Aqswa aonya kuhusu siasa hatarishi za wavamizi

Khatibu wa Msikiti wa Al-Aqswa ameonya kuhusiana na kushadidi mashambulizi ya Wazayuni dhidi ya Msikiti wa Al-Aqswa na Baytul Muqaddas, na na kutoa mwito wa kukabiliana mara moja na vitendo hivyo visivyo vya kibinadamu.

Sheikh Ekrima Sabri, Khatibu wa Msikiti wa Al-Aqswa, ametaka  kuchukuliwa hatua za haraka na za maana katika nyuga zote kwa ajili ya kukabiliana na mipango michafu ya wavamizi ya Msikiti wa Al-Aqswa na mji wa Quds.

Aidha amesema, utawala wa Kizayuni wa Israel umepanua wigo wa uvamizi wake dhidi ya Masjdul Aqswa tangu kulipianza vita vya Gaza.

Sheikh Sabri amebainisha kwamba, wavamizi wanatekeleza siasa za kuwabaidisha kwa umati Wapalestina jambo ambalo halifanyika sehemu yoyote ile duniani.

Khatibu wa msikiti wa al-Aqswa aonya kuhusu siasa hatarishi za wavamizi

Msikiti wa al-Aqswa unajulikana kuwa nembo kuu ya utambulisho wa Kiislamu na Kipalestina wa eneo takatifu la Quds na utawala wa Israel unajaribu kuharibu utambulisho huo, lakini kusimama imara na kuwa macho wananchi wa Palestina kumeufedhehesha utawala huo wa Kizayuni na kupelekea njama zake kushindwa.

Walowezi wengi wa Kizayuni wenye misimamo mikali mara kwa mara wamekuwa wakivamia msikiti wa al-Aqswa kibla cha kwanza cha Waislamu na kufanya vitendo vya kichochezi huku wakiwa wanapatiwa ulinzi na vikosi vya usalama vya utawala haramu wa Israel.

Vitendo vya hujuma za walowezi wa Kizayuni dhidi ya msikiti wa al-Aqswa vimekithiri zaidi baada ya kuingia madarakani serikali yenye misimamo mikali ya Benjamin Netanyahu ambayo imekuwa ikionyesha chuki za wazi wazi dhidi ya Wapalestina na maeneo yao matakatifu.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha