2 Agosti 2015 - 19:29
 Jeshi la Iran liko makini kulinda mipaka ya lao

Kamanda mkuu wa jeshi la Ardhi la jamhuri ya Kiislamu ya Iran alipokuwa anaashiria matukio ya mashariki ya kati amesema: jeshi la Ardhi la Iran liko makini na harakati zote zinazojiri katika mashariki ya kati na laakidisha kuwa inasimamia mipaka yake ipasavyo.

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: kamanda wa jeshi la Ardhi la jamhuri ya Kiislamu ya Iran baada ya kubainisha matukio yanayojiri mashariki ya kati amesema: jeshi letu limejiimarisha zaidi katika kulinda mipaka ya taifa na laakidisha linakabiliana na hatua zote za maadui dhidi ya jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Ahmad Ridha Purdastan amebainisha kuwa majemadari wa taifa hilo hutumia ushujaa wao wote kuhakikisha mipaka ya mchi yao iko salama kutokana na maadui walio dhidi ya serikali hiyo.
Aidha amesema: endapo ikashuhudiwa hatua yeyote inayo hatarisha amani ya taifa letu tutaingia kimapambano kwa vishindo vikubwa kuhakikisha tunawasambaratisha maadui hao, kwani hivi sasa majeshi ya Iran yamezidi kuwa na umoja na mshikamano katika kila nyanja, hivyo endapo tukaona ishara ndongo inayoashiria hatari katika nchi yetu tutaipatia jawabu zito ambalo haitawaacha salama maadui hao.
Akibainisha kuwa maadui zetu wanafahamu vizuri umakini wa jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika masuala ya kivita huku akisisitiza kuwa kwa sasa maadui wa jamhuri ya Kiislamu ya Iran hawawezi kuanzisha vita ya moja kwa moja na Iran, bali hutumia njia ya kutengeza vikundi vya kigaidi wakifikiria vitaweza kukabiliana na nguvu ya taifa letu.
Naye amesema kuwa jeshi la Kiislamu la Iran lilipigana miaka minane huku wakiwa na vikwazo lakini waliweza kukabiliana na changamoto zote mpaka kushinda vita, na mpaka sasa tumefanikia kuzalisha vifaa vya kivita vya hali ya juu.