7 Septemba 2015 - 18:06
Zarif: Wananchi wa Syria ndio pekee wanahaki  ya kumchagua Rais wanaomtaka

Waziri wa mambo ya nje wa Iran amesema: masuala ya Syria yanabidi yatatuliwe kwa mazungumzo ya kisiasa, na kuhusu suala la Rais wa nchi hiyo, wanachi pekee ndio wana haki ya kuchukua maamuzi kwamba nani anawafaa

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: kwamujibu wa shirika la habari la Irna, waziri wa mambo ya nje wa Iran (Mohammad Javad Zarif) ameashiria hayo siku ya Jumatatu katika mkutano wapamoja na vyombo vya habari pamoja na wazi wa mambo ya nje wa Ispania uliofanyika katika wizara ya mambo ya nje mjini Teheran amesema: wale ambao wameweka masharti kunako suala la Rais wa Syria ndio wanasababisha kuendelea kwa vita nchini humo, kwamaana badala ya wananchi wa nchi hiyo kumchagua Rais wanaemtaka, wao hulazimasha kutumika matashi yao katika taifa hilo kitu ambacho kinasababisha kuendelea umwagaji wa damu za wananchi wa nchi hiyo.
Aidha katika kusisitiza njia ya utatuzi wa mgogoro wa Syria kuwa si njia ya kivita na kijeshi amesema: mtazamo wa Iran na Ispania katika kutatua mgogoro wa Syria utawezekana kwa kutumia njia ya mazungumzo ya amani na upendo, huku tukiamini kuwa mgogoro huo utatuliwa kupitia wananchi wa nchi hiyo.
Mohammad Javad Zarif amesema: wanao lazimisha matashi yao nchini humo wanapaswa kuacha kutumia maoni yao katika kuwalazimisha wananchi wa nchi hiyo haraka iwezekanvyo, hatimaye kuwaanchia wanchi kujichagulia Rais na kiongozi wanaemtaka kwaajili ya kulitumikia taifa hilo na kuleta umoja na mshikamano katika taifa lao katika kila sekta.
Naye amebainisha kuwa: indapo njia hii itatumika, ninamini kuwa matatizo yaliopo nchini humo yatakwesha, kwa sharti kuwa mataifa ya kigeni yasilazimishe matashi yao kwaajili ya kupata manufaa yao yamuda mfupi nchini humo kwa kuwatumia wanachi hao, badala yake kuyaacha matashi ya wananchi yafanye kazi yake.
Pia amesema: sisi tunasisitiza utatuzi wa mgogoro wa nchi hiyo kwa njia ya mazungumzo ya kiasiasa na  amani ambapo ndio njia pekee ya kumaliza mgogoro wa nchi hiyo, nao wanapaswa kusahau ndoto yakuamini kuwa mgogoro huo utatatuliwa kwa njia ya nguvu za kijeshi.
Mwisho wa Habari/290