5 Oktoba 2015 - 22:16
 Askari wa Israel wamuua mdogo wa Palestina

Kijana mdogo wa kipalestina ameuliwa na askari wa Israel hii leo karibu na mji wa Bethlehem, katika ukingo wa magharibi wa mto Jordan.

Shirika la  habari la ABNA linaripoti kuwa: Kijana mdogo wa kipalestina ameuliwa na askari wa Israel hii leo karibu na mji wa Bethlehem, katika ukingo wa magharibi wa mto Jordan. Duru za hospitali za Palestina zimesema. Kijana huyo mwenye umri wa miaka 13 alikuwa akiishi katika kambi ya wakimbizi ya Al Aidah. Amepigwa risasi juu ya moyo. Jeshi la Israel linasaema halijui chochote kuhusu tukio hilo na linasema litalichunguza. Matumizi ya nguvu yamepamba moto mnamo siku za hivi karibuni huko Jerusalem ambako ni mji mkuu wa Palestina na katika ukingo wa magharibi kutokana na hali tete iliyoko katika eneo la Harami  Sharif unakokutikana msikiti wa Al Aqsa. Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameahidi hapo jana kupitisha hatua kali juu ya kile anachokiita kuwa ni kukabailiana na wapalestina wanaohusika na mashambulio dhidi ya waisrael.

Mwisho wa habari/291