Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: jeshi la Yemen likiungana na majeshi ya wananchi ya kujitolea siku ya Alhamisi wamefanikiwa kulikombo eneo kubwa liliopo katika fukwe za bahari nyekundu nchini Yemen.
Kwa mujibu wa ripoti hii jeshi na nguvu za wananchi katika mwendelezo wake wa kuyakomboa maeneo muhimu ya fukwe za bahari nyekundo kuelekea upande wa kusini mwa mkoa wa Taiz ambapo kulifanyika mashambulizi makali baina ya majeshi ya Yemen na kikundi cha Rais wa zamani wa nchi hiyo hatiamye kuikomboa sehemu hiyo.
Mapambano makali yalifanyika katika sehemu muhimu iitwayo (Muthalathu Al-amri) ambapo pia ni karibu na kambi ya kijeshi ya Al-amri kwa kilometa mbili.
Jambo muhimu la kukumbushia hapa ni kwamba sehemu ya Bab el-Mandeb mpaka sasa mara kadhaa ilishawai kuingia mikononi mwa majeshi ya Yemen na kikundi cha Rais wa Zamani Mansuri Alhadi, ambapo mpaka sasa bado inagombaniwa sehemu hiyo muhimu, lakini hali ya mazingira yanaashiria kuwa jeshi la Yemen na nguvu za wananchi wataweza kuimiliki sehemu hiyo hivi karibuni.
8 Januari 2016 - 11:20
Msimbo wa Habari: 729446
Majeshi ya Yemen wamefanikiwa kusonga mbele katika ufukwe wa bahari nyekundu na kuikaribia sehemu muhimu ya Bab el-Mandeb