21 Februari 2016 - 18:41
 Raia wa Comoro wanachagua rais

Wapiga kura katika visiwa vya Comoro wameanza kupiga kura kuchagua rais mpya katika uchaguzi wenye kujumuisha wagombea 25

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Wapiga kura katika visiwa vya Comoro wameanza kupiga kura kuchagua rais mpya katika uchaguzi wenye kujumuisha wagombea 25, ambapo ukuzaji wa uchumi na miundombinu duni zikiwa ajenda kubwa. Vituo vya kupiga kura katika taifa hilo lenye watu wasiozidi milioni moja vilifunguliwa rasmi mapema asubuhi, ingawa katika baadhi ya maeneo vilichelewa kufunguliwa kutokana na kuchelewa kufika kwa vifaa vya kupigia kura. Miongoni mwa wanaowania nafasi hiyo katika duru ya kwanza ni pamoja na makamo wa rais na kiongozi wa zamani wa mapinduzi ambaye aliwahi kuwa rais mara mbili. Ni wapiga kura wa kisiwa cha Ngazija tu, ndio watakaopiga kura leo, katika mfumo usio wa kawaida, wenye kuamuru kwamba rais anachaguliwa kwa mtindo wa kupokezana miongoni mwa visiwa vitatu vinavyounda taifa hilo. Wagombea watatu watakaoibuka kifua mbele katika uchaguzi huu, watachuana tena Aprili, uchaguzi ambao utaamua nani atakuwa mrithi wa Rais Ikililou Dhoinine.

Mwisho wa habari/ 291