Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Muungano wa mataifa yanayosaidia waasi ili kuendeleza machafuko nchini Syria kwa lengo la kumtoa madarakani rais Bashar asad wanakutana leo kujadili mbinu mpya za kufanya.
Mataifa 11 washirika wa muungano unaoongozwa na Marekani kwa madai ya kupambana dhidi ya kundi la kigaidi la Daesh nchini Iraq na Syria, yanafanya mkutano wao mjini Stuttgart leo kuweka mikakati juu ya kuongeza usaidizi kwa Iraq.
Mikakati hiyo ni juhudi za kuisaidia Iraq kuukamata tena mji wa Mosul ambao ni ngome kuu ya kundi la kigaidi la Daesh .
Kikao hicho ni cha hivi karibuni kabisa katika mlolongo wa mikutano kama hiyo ya washirika kuweka mikakati ya kuongeza usaidizi kwa Iraq ili kuikamata ngome ya kundi la kigaidi la Daesh upande wa kaskazini mwa Iraq ya Mosul, lakini jeshi la wanamgambo wa kishia la Iraq linapinga muungano huo wa Marekani kutokana na muungano huo kuwasaidia magaidi.
Hii inakuja wakati mzozo wa kisiasa katika serikali ya mjini Baghdad unaweka kiwingu katika muonekano wa mafanikio zaidi ya kijeshi dhidi ya wanagambo wa kundi la kigaidi la Daesh.
Waziri wa ulinzi wa Marekani Ash Carter amesema wakati akiwasili mjini Stuttgart kuhudhuria mkutano huo kwamba kifo cha mwanajeshi wa Marekani katika mapambano nchini Iraq kinaonesha kwamba kampeni ya kijeshi dhidi ya kundi la kigaidi la Daesh, "bado hayajaisha."
Marekani yawataka washirika wake kuweka nguvu zaidi
Carter ameweka umuhimu wa juu katika kuwavuta washirika ndani zaidi ya kampeni ya kupambana na kundi la kigaidi la Daesh, akisisitiza kitisho kilichopo kwa kuwaruhusu wanamgambo hao wenye itikadi kali kusambaza ushawishi wao.
kundi la kundi la kigaidi la Daesh lilimuua mwanajeshi wa Marekani kaskazini mwa Iraq jana Jumanne baada ya kupiga katika ngome za ulinzi za wapiganaji wa Kikurdi na kuukamata mji mmoja katika shambulio kubwa katika eneo hilo kwa muda wa miezi kadhaa, wamesema maafisa.
Mwanajeshi huyo anakuwa wa tatu kutoka marekani kuuwawa katika mapambano ya moja kwa moja tangu muungano unaoongozwa na Marekani kuanzisha kampeni hiyo mwaka 2014 "kuharibu ili kuvuruga uwezo" wa kundi la kigaidi la Daesh na ni hatua ya kuingia zaidi katika mzozo huo.
"Ni kweli kwamba ni kifo katika mapambano , na ni kifo kinachosikitisha," amesema waziri wa ulinzi wa Marekani Ashton carter wakati alipokuwa akizungumza na waandishi habari wakati wa ziara nchini Ujerumani.
Marekani yatuma Kikosi cha SEAL
Afisa wa wizara ya ulinzi ya Marekani , akizungumza kwa masharti ya kutotajwa jina , amesema mwanajeshi huyo aliyeuwawa alikuwa katika kikosi maalum cha SEAL.
Wanajeshi wa kikosi hicho wanaonekana kuwa miongoni mwa wanajeshi maalum wa Marekani wenye uwezo mkubwa na wanaoweza kuingia katika maeneo hatari. Jina na cheo cha mwanajeshi huyo havikutajwa na wizara ya ulinzi ya Marekani.
Ikumbukwe kuwa wanajeshi wa kikosi hiki walisha wahi kukamatwa na jeshi la Iran pindi walipovuka mipaka ya Iran, jambo liliifanya Marekani kuona kuwa imedhalilishwa kutokana na jinsi wanajeshi hawa wanaosifika walivyokamatwa bila ya taharuki.
Gavana wa jimbo la Marekani la Arizona , Doug Ducey , alimtaja mwanajeshi huyo aliyeuwawa kuwa ni Charlie Keating IV, na kusema Keating alihudhuria masomo yake ya juu katika shule mjini Phoenix.
Gazeti la San Diego Union-Tribune , la califonia kusini, limemweleza mwanajeshi huyo ambaye hakutajwa na ndugu zake katika taarifa yake kuwa Keating alikuwa ni mjukuu wa Charles Keating Jr.,mfanyakazi wa benki ambaye alikuwa mstari wa mbele katika kashfa ya masuala ya kuweka akiba na mikopo nchini Marekani ya miaka ya 1980 ambayo iliwahusisha maseneta watano wa Marekani.
Muungano wa kijeshi unaongozwa na Marekani ambao unadai kupambana na kundi la kigaidi la Daesh, umekuwa ukiwafunza wanamgambo kutoka nchi mbalimbali mafunzo ya kijeshi na kuwapatia silaha na kupeleka Syria kwa lengo la kupambana na serikali ya Syria, vikundi vya wanamgambo hawa Marekani inaviita kuwa ni vikundi vya waasi sio vya kigaidi, wapiganaji wa wengi vikundi hivi wamejiunga na kundi la kigaidi la Daesh ambalo Muungano wa Marekani na washirika wake linadai kupambana na kundi hilo kwa miaka minne sasa bila mafanikio.
Muungano mpya wa kijeshi ambao unaongozwa na Urusi ambao umekusanya wataalamu wa vita kutoka Iran, wanajeshi wa Syria na wapiganaji wa kundi la Hizbullah umepata mafanikio makubwa dhidi ya makundi ya kigaidi nchini Syria, jambo lililopelekea Muungano wa Marekani na nchi 11 kuuchukia Muungano huo ambao hauungi mkono waasi wala magaidi badala yake unapambana na magaidi wote hata wale ambao Marekani inadai kuwa ni waasi.
Marekani na washirika wake sasa wameacha kutangaza mauaji yanayofanywa na makundi ya kigaidi nchini Syira na kugeuza kibao na kusema kuwa majeshi ya Urusi yanashambulia raia nchini Syria.
Urusi imesema haitaruhusu Marekani na washirika wake, wasababishe machafuko nchini Syria kama walivyofanya Libya kwa utawala wa Muamar Gaddafi.
Mwisho wa habari/ 291