11 Mei 2016 - 18:45
Jasusi wa kike wa Urusi anyongwa

Jarida la Daesh la lugha ya kirusi ambalo linasambazwa katika mitandao limeandika katika chapa yake ya mwisho kuwa baada ya uchunguzi mkali uliofanyika wamemkamata jasusi mmoja wa kike wa Urusi na hatimaye kumyonga.

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: kikundi cha kigaidi cha Daesh kimedai kumkamata jasusi wa kike wa Urusi na hatimaye kumyonga.
Katika habari hii kikundi cha kigaidi cha Daesh kimesema jina la jasusi huyo kuwa ni “Alwira Karyova” ambaye alikuwa anashirikiana na viongozi wakuu wa kikundi hicho cha kigaidi, ambapo alifanikiwa kuuwa watu kadhaa wa kikundi cha Daesh, ama mwisho wake walimfahamu kupitia majasusi wa kikundi cha kigaidi cha Daesh na hatimaye kumyonga.
Jarida la Daesh la lugha ya kirusi limedai kuwa Alwira ni jasusi wa Urusi ambaye kwa muda wa miaka minne alikuwa akijishughulisha na ujasusi katika kikundi cha kigaidi cha Daesh kwaajili ya Urusi.
Kazi aliokuwa akiitekeleza katika ujasusi wake ilikuwa ni kuchukua ripoti zinazohusu wanachama wa kigaidi cha Daesh na kueleza sehemu waliopo magaidi hao ikiwemo na kutuma picha zao kwenda katika serikali ya Urusi.
Kwamujibu wa makala ilioandikwa katika jarida hilo ni kama ifuatavyo: kazi ya Alwira ilipelekea kushakiana baina ya viongozi wa kikundi cha Daesh, huku akifanikiwa jasusi huyo kupitia uhakiki wake kudhoofisha kikundi cha kigaidi cha Daesh, kwani magaidi hawakuwa wanahisi kuwa wanafanyiwa uchunguzi na uhakiki.
Lakini baada ya muda kupita majasusi wa kikundi cha kigaidi cha Daesh walianza kufanya uhakiki wa kina kuhusu mtu huyo anayetoa ripoti za kwa serikali ya Urusi, na mwisho wakamgundua na baada ya kukiri ujasusi wake wakamuhukumu kinyongo.
Mmoja katika ya watu muhimu wa Daesh amesema kuwa: Alwira ni katika Warusi waliokiuka dini ambaye alikuwa akitoa ripoti za wanajihadi kwa serikali ya Urusi, na sasa ameshatiwa mikononi na ameyaona matunda ya kazi yake.
Baada ya kupita masiku kadhaa baada ya kikundi cha kigaidi cha Daesh kutangaza habari hii mpaka sasa serikali ya Urusi haijathibitisha aua kukanusha suala hilo.  
mwesho wa Habari/290