Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: majeshi ya Syria yamefanikiwa kupata ushindi mwingine mkubwa dhidi ya kikundi cha kigaidi cha Daesh nchini humo.
Majeshi ya serikali ya Syria katka mji wa Homeh kusini mwa mji wa “Tabaqeh” katika Mkoa wa Raqqah ambapo wamefanikiwa kusonga mbele na wamefanikiwa kufika katika makutano ya Raswafeh na Tabaqeh na kukimiliki kisima cha mafuta cha Swafiyeh na kuzikomboa sehemu hizo.
Aidha jeshi hilo mpaka hivi sasa zimebaki kilometa 15 kufika katika kambi kuu ya Daesh katika mkoa wa Raqqeh nchini Syria.
Katika mashambulio ya masiki haya karibuni majeshi ya Syria katika mkoa wa Raqqeh wame waangamiza magaidi zaidi ya 80 katika mji huo.
Mkoa wa Raqqeh hasa wilaya ya Raqqeh ndio makao makuu ya asili ya kikundi cha kigaidi cha Daesh nchini Syria, na maeneo hayo yalimilikiwa na kikundi cha hicho cha kigaidi zaidi ya miaka miwili.
mwisho wa Habari/290