Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Serikali ya Uturuki imeamuru kufungwa kwa vyombo kadhaa vya habari yakiwemo mashirika ya habari, vituo vya matangazo kwa njia ya televisheni na radio pamoja na magazeti. Serikali ya nchi hiyo pia imetoa waranti wa kukamatwa kwa waandishi kadhaa wa habari ikiwa ni sehemu ya operesheni inayoendelea ya kuwatia mbaroni watu wanaoshukiwa na kuhusika na jaribio la mapinduzi lililoshindwa la Julai 15, mwaka huu. Waziri Mkuu wa Uturuki, Binali Yildirim hapo jana ameonya kuwa operesheni hiyo haijafika mwisho kutokana na serikali ya nchi hiyo kutoa waranti wa kukamatwa kwa wafanyakazi kadhaa wazamani wa magazeti. Zaidi ya watu 15,000 tayari wametiwa mbaroni wakihusishwa na jaribio hilo la mapinduzi lililoshindwa.
Serikali ya Uturuki imehusishwa na mauaji ya kinyama dhidi ya watuhumiwa wanaoshukiwa kushiriki mapinduzi hayo.
Mwisho wa habari/ 291