Ubalozi wa China (katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni) Israel umesasisha uainishaji wa maeneo hatari kwa usalama huko Israel, ikiyaorodhesha maeneo fulani kuwa nyekundu (ya hatari sana) na mengine kuwa ya machungwa (hatari kubwa).
Wizara ya Mambo ya Nje imewataka raia wa China kuwa waangalifu, kufuatilia kwa karibu yanayojiri, kuimarisha tahadhari za usalama na kuwa tayari kwa dharura. Imesema iwapo watakabiliwa na dharura, wanapaswa kuwasiliana na polisi wa ndani na Ubalozi wa China.
Haya yanajiri wakati huu ambapo Jeshi la Yemen limeendelea kuutwangwa kwa makombora ya balestiki na droni uwanja wa ndege wa Ben Gurion wa utawala wa Kizayuni huko Tel Aviv.
Msemaji wa Jeshi la Yemen, Brigedia Jenerali Yahya Saree amesema vipigo vya jeshi la Yemen dhidi ya maeneo nyeti na muhimu mno ya Israel vitaendelea hadi utawala wa Kizayuni utakapokomesha jinai zake huko Ghaza na kuacha kuuzingira ukanda huo.
Amesisitiza kuwa, operesheni hizo ni sehemu ya kuliunga mkono taifa madhlumu la Palestina hasa wananchi wa Gaza na kujibu jinai na mauaji ya kimbari yanayofanywa na Israel dhidi ya watu hao wasio na ulinzi.
Your Comment