24 Mei 2025 - 22:49
Source: Parstoday
Kwa nini mauaji ya kimbari yangali yanaendelea licha ya uungaji mkono wa kimataifa kwa Gaza?

Nchi 80 zimetangaza kupitia taarifa kwamba: 'Ukanda wa Gaza unakabiliwa na mzozo mbaya zaidi wa kibinadamu tangu Oktoba 7, 2023, na raia wako katika hatari ya kupoteza maisha kutokana na baa la njaa. Jinai na mauaji ya kimbari ya utawala wa Kizayuni yangali yanaendelea huko Gaza.'

Jinai hizo zinaendelea huku watu wa Gaza wakiendelea kukabiliwa na tatizo la usalama wa chakula, ambapo asilimia 92 ya watoto wanakumbwa na baa la njaa na utapiamlo, majiko ambayo wakazi wa Gaza wanayategemea kwa madhumuni ya kuandaa chakula yameharibiwa na chakula hakipatikani katika maghala ya mashirika ya misaada, vituo vya usambazaji chakula wala masoko.

Wakati huo huo, Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imetangaza kupitia mtandao wa kijamii wa X kwamba takriban asilimia 81 ya maeneo ya Ukanda wa Gaza ama yako chini ya udhibiti wa majeshi ya Israel au wakazi wameamrishwa kuhama.

OCHA imesisitiza kuwa Wapalestina 160,000 wamelazimishwa tena kuyahama makazi yao katika kipindi cha wiki iliyopita ambapo wanakabiliwa na mashambulizi makali ya mabomu huku wakiwa hawana makazi, chakula wala vifaa vya msingi vya kuendeshea maisha.

Umoja wa Mataifa pia umetahadharisha kuhusu maafa ya kibinadamu huko Gaza.

Sasa swali ni je, kwa nini, licha ya uungaji mkono huu wote wa kimataifa kwa Gaza lakini bado mauaji ya halaiki yanaendelea kufanywa na utawala wa kibaguzi wa Israel dhidi ya Wapalestina wasio na hatia katika ukanda huu?

Sababu kadhaa zinaweza kutolewa katika kujibu swali hili. Ni wazi kuwa kutoadhibiwa watawala wa Israel kutokana na jinai za kutisha wanazofanya dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza na kujiona kuwa wako juu ya sheria kuhusu suala hilo, ni moja ya sababu muhimu zaidi za kuendelea mauaji hayo ya kimbari na jinai ambazo hazijawahi kushuhudiwa katika historia.

Your Comment

You are replying to: .
captcha