24 Mei 2025 - 22:49
Source: Parstoday
HAMAS: Ukanda wa Gaza unakabiliwa na hali mbaya kabisa ya mgogoro wa kibinadamu

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) imetangaza katika taarifa yake kwamba, Ukanda wa Gaza unakabiliwa na hali mbaya kabisa ya mgogoro wa kibinadamu.

Taarifa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (HAMAS) imeeleza kuwa, taarifa iliyotolewa na nchi 80 inasisitiza juu ya kupanuka upinzani wa kimataifa dhidi ya jinai na mauaji ya kimbari dhidi ya watu wa Gaza.

Harakati ya Hamas imepongeza na kukaribisha taarifa ya pamoja ya nchi 80 iliyosema kuwa, Ukanda wa Gaza unakabiliwa na mgogoro mbaya zaidi wa kibinadamu tangu kuanza hujuma ya Israel dhidi yake Oktoba 2023. Taarifa hiyo ya pamoja pia imesisitiza haja ya kuwalinda watu wasio na ulinzi wa Ukanda wa Gaza kwa mujibu wa sheria za kimataifa.

Hamas imebainisha kuwa, sisitizo la nchi themanini katika tamko la pamoja la kupinga matumizi mabaya wa misaada ya kibinadamu kwa malengo ya kisiasa, kijeshi au kiusalama kunahitaji mashinikizo makali dhidi ya utawala wa Kizayuni kwa ajili ya kuwaunga mkono wananchi wa Gaza, kusimamisha vita vya njaa na kuvunja mzingiro wa kikatili uliowekwa dhidi yao.

Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (Hamas) imezitaka nchi zote za dunia kulaani jinai zinazoendelea za utawala wa Kizayuni dhidi ya wananchi wa Palestina, na kuchukua hatua madhubuti za kuuadhibu utawala huo wa Kizayuni, na kuilazimisha serikali ya kijinai na kivita ya Netanyahu kusimamisha hujuma hizo za kinyama na kuwajibishwa kwa kutenda jinai dhidi ya binadamu.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha