27 Mei 2025 - 23:33
Source: Parstoday
Vyama vya upinzani Ugiriki vyaitaka serikali isitishe ushirikiano wa kijeshi na Israel

Vyama vya upinzani nchini Ugiriki vimeitaka serikali ya nchi hiyo isitishe ushirikiano wake wa kijeshi na utawala wa Kizayuni wa Israel

Taarifa ya vyama vya upinzani vya mrengo wa kushoto vya Ugiriki imeitaka serikali kusimamisha ushirikiano wa kijeshi na utawala wa Kizayuni na kuitambua Palestina kama taifa.

Vyama vya Syriza, Greece Communist, New Left na Course of Freedom kwa pamoja vimeandika barua kwa Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ugiriki, vikitoa wito wa kusimamishwa ushirikiano wa kijeshi wa Athens na utawala wa Kizayuni na kutambuliwa a Palestina kama taifa.

Barua hiyo pia inasema: "Kila siku na kwa kiwango kikubwa, vitendo vya mauaji ya halaiki, uhalifu dhidi ya ubinadamu na uhalifu wa kivita vinatokea huko Gaza, vitendo ambavyo vinakiuka kila dhana na kifungu cha sheria za kimataifa, sheria za kimataifa za kibinadamu na sheria za kimataifa za jinai.

Sehemu nyingine ya barua hiyo inasema: "Hatua za utawala wa Kizayuni zinakinzana kabisa na hisia za watu duniani kote wakiwemo wananchi wa Ugiriki ambao mara kwa mara wamekuwa wakionyesha mshikamano wao na wananchi wa Palestina.

Kadhalika vyama hivyo vya upinzani nchini Ugiriki vimesema katika barua yao hiyo: Kutokana na matukio haya yote muhimu, serikali ya Ugiriki haina haki ya kisiasa, kisheria au kimaadili kuhalalisha na hatimaye kuunga mkono uhalifu huu.

Kwa kuzingatia mazingira haya, vyama hivyo vya upinzani vimetoa wito kwa serikali ya Athens kufanya juhudi ili kuhakikisha usitishaji wa mapigano mara moja huko Gaza na kupelekwa misaada ya kibinadamu bila kipingamizi katika eneo hilo lililozingirwa.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha