Kwa mujibu wa Rai al-Youm, kitu cha kushangaza ni kwamba machafuko yalizuka wakati wa usambazaji wa chakula cha makopo na licha ya kufyatuliwa risasi na maafisa wa Marekani, watu waliingia katika kituo hicho na kukiharibu na kuchukua chakula, na maafisa wa Marekani walijifanya kukimbia licha ya kwamba walikuwa na silaha.
Mtaalamu wa Palestina, Ahmed al-Najjar amesema kuwa, kilichotokea Rafah jana (Jumanne) si machafuko bali ni njama iliyopangwa vyema ya kuwalazimisha watu wa Ghaza kuhama kwenye ardhi zao.
Ameongeza kuwa: Madhumuni ya kuzusha machafuko bandia kama hayo ni kuwalazimisha watu wa Ghaza kuhamia kwenye Jangwa la Sinai nchini Misri. Kwa hiyo, Misri lazima ielewe njama hiyo ya Marekani, iunge mkono utulivu wa watu wa Ghaza na isiruhusu kuhamishwa kwa nguvu kutoka kwenye maeneo yao.
Kwa upande wake mwandishi Mpalestina Mohamed al-Jundi ametahadharisha kwamba machafuko hayo bandia yaliyotokea jana huko Rafah, kusini mwa Ghaza, huenda yakawa ni utangulizi wa kuwaondoa watu wa Ghaza na kuwapeleka kwenye jangwa la Sinai nchini Misri ili kukamilisha njama za muda mrefu za kuwahamisha Wapalestina kwenye ardhi zao. Njama hizo hivi sasa zinaendeshwa kwa mauaji ya umati na ukatili wa kuchupa mipaka unaofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya watu wa Ghaza.
342/
Your Comment