28 Mei 2025 - 20:13
Source: Parstoday
Siku 600 za mauaji ya kimbari Gaza; Hamas yaitisha maandamano

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imetoa wito kwa Wapalestina, Waarabu, Waislamu na watu huru kote duniani kushiriki katika harakati ya kimataifa na maandamano ya 'ghadhabu za kimataifa' kuadhimisha siku 600 za "mauaji ya halaiki na njaa" dhidi ya watu wa Gaza.

Katika taarifa iliyotolewa Jumanne, Harakati ya Muqawama wa Palestina imekariri wito wake wa "sauti za kimataifa zipazwe kulaani mauaji ya kimbari na njaa ya utawala wa Israel dhidi ya raia wasio na ulinzi, watoto na wanawake."

Kundi hilo la Muqawama limehimiza mashirika na taasisi duniani kote "kuongeza aina zote za hatua za kimataifa, katika miji na viwanja kote ulimwenguni, dhidi ya uchokozi, maangamizi, na njaa inayolenga watu wetu."

"Tunatoa wito wa maandamano ya kimataifa kukomesha mara moja mauaji ya Wazayuni. Siku zijazo na ziwe siku za ghadhabu ya kimataifa," Hamas imesema, ikitoa wito wa "maandamano, mikusanyiko, na migomo ya kuketi chini."

Kadhalika harakati hiyo imesema katika taarifa yake kuwa: "Tunatoa wito kwa taifa letu, Umma wa Kiarabu na Kiislamu, na watu huru kote duniani, kufanya maandamano na kushiriki katika matukio ya kuonyesha mshikamano (na Wapalestina) katika miji na viwanja mbalimbali duniani, ili kupinga mipango ya kuwaondoa watu wetu wa Palestina kutoka katika ardhi yao."

Hali kadhalika Harakati ya Muqawama ya Hamas imesisitiza kuwa inathamini misimamo ya kimataifa katika kuonyesha mshikamano na Wapalestina katika Ukanda wa Gaza. Katika miezi ya hivi karibuni, miji duniani kote imeshuhudia wimbi la maandamano makubwa na maandamano ya mshikamano na Palestina.

Israel ilianzisha mashambulizi yake ya kinyama dhidi ya Gaza mnamo Oktoba 7, 2023. Tangu wakati huo, zaidi ya Wapalestina 54,000 wameuawa shahidi, wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto, kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Gaza.

Your Comment

You are replying to: .
captcha