Pezeshkian ameyasema hayo kwenye mazungumzo ya simu na Amir wa Kuwait, Mishal al-Ahmad al-Jaber al-Sabah, jana Jumatano, akitoa salamu za Idd al-Adh'ha kwa serikali na watu wa Kuwait.
Akisisitiza mafungamano ya kidini, kiutamaduni na kihistoria baina ya mataifa ya Kiislamu, Pezeshkian amesema, kwa kuzingatia mafundisho ya Mtume Muhammad (SAW), Iran inazichukulia nchi zote za Kiislamu na Waislamu duniani kote kuwa ni ndugu zake na kuongeza kuwa, kuimarisha uhusiano na umoja ndani ya Umma wa Kiislamu ni wajibu wa kidini na wa kistratijia.
Rais pia alilaani jinai zinazoendelea kufanywa na Israel dhidi ya Gaza, akisisitiza kwamba juhudi zinapaswa kufanywa ili kukomesha ukandamizaji na hatimaye kupatikana haki kwa watu wa Palestina. Wakati wa mazungumzo hayo, al-Sabah pia ilitoa salamu za Iddi, akilitakia taifa la Iran amani, afya, na fanaka, pamoja na mataifa yote ya Kiislamu.
Rais Masoud Pezeshkian na Amir wa Qatar Tamim bin Hamad Al Thani
Wakati huo huo, Rais Masoud Pezeshkian na Amir wa Qatar Tamim bin Hamad Al Thani wamesisitiza haja ya juhudi za pamoja za kumaliza vita vya mauaji ya halaiki ya Israel katika Ukanda wa Gaza.
Katika mazungumzo ya simu na Tamim bin Hamad Al Thani siku ya Jumatano, Rais Pezeshkian ametoa wito wa kuwepo ushirikiano zaidi wa kidiplomasia na kisiasa kati ya mataifa ya Kiislamu ili kuushinikiza utawala wa Israel ukomeshe jinai na ukandamizaji wake dhidi ya watu wasio na ulinzi wa Gaza na kurejesha amani katika eneo hilo. Pezeshkian pia ametoa mkono wa Idd al-Adh'ha kwa watu na serikali ya Qatar, akiwatakia mafanikio.
Kadhalika Sultan Haitham bin Tariq wa Oman ametoa pongezi zake za dhati kwa mnasaba wa Sikukuu ya Idd al-Adh'ha na kusisitiza umuhimu wa kuimarishwa uhusiano mkubwa wa pande mbili kati ya Oman na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Rais wa Iran na Amir wa Kuwait, Mishal al-Ahmad al-Jaber al-Sabah
Katika mazungumzo ya simu na Rais Masoud Pezeshkian jana Jumatano, Sultan Haitham aliwasilisha salamu zake kwa utawala na watu wa Iran, akitakia kheri na baraka mataifa yote mawili na ummah mpana wa Kiislamu.
Sultan wa Oman alielezea kuridhishwa na mazungumzo ya hivi majuzi yaliyofanywa na Rais Pezeshkian huko Muscat na kubainisha kuwa, ushirikiano wa nchi hizi mbili una sifa ya kipekee na unaoendelea kustawi.
Your Comment