15 Juni 2025 - 15:59
Safari za ndege zimehairishwa hadi ilani nyingine/Shule, Misikiti, na njia za chini ya ardhi zitafunguliwa kwa umma saa 24 kwa siku kuanzia leo usiku

Msemaji wa Serikali amesema: "Hakuna shida katika kusafirisha bidhaa, dawa, chakula, na mahitaji ya watu, haswa mafuta."

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-, Fatimeh Mohajerani katika mahojiano ya televisheni alisisitiza kuwa kutokana na hali ya vita inayoendelea nchini, safari za ndege zimesitishwa hadi itakapotangazwa tena, na akasema: "Bila shaka hakuna tatizo katika kusafirisha bidhaa, dawa, chakula na mahitaji ya watu hususan mafuta."

Vile vile ametoa salamu za rambirambi kwa kuuawa shahidi raia kadhaa wakiwemo zaidi ya Wanawake 30 na watoto na kuongeza kuwa: "Tukio hili la kuua wananchi wa kawaida limetokea licha ya madai ya uongo ya utawala wa Kizayuni."

Tutazungumza na wananchi kila siku kwenye vyombo vya habari vya kitaifa

Mohajerani aliendelea: Tutazungumza na watu kila siku kwenye vyombo vya habari vya kitaifa chini ya anuani hii: "Kuzungumza na Wananchi."

Msemaji wa serikali alikumbusha: Katika saa za kwanza za uchokozi huu wa wazi, serikali ilifanya mkutano rasmi na kisha kufuatilia kazi yake maalum kwa njia isiyo rasmi. Mawaziri pia wanafuatilia na kamati nne zimeundwa.

Mohajerani aliongeza: “Kamati ya miundombinu ambayo majukumu yake makuu ni pamoja na kusimamia urejeshwaji wa mahujaji, imefanya uratibu mzuri na Waziri wa Barabara, na suala hili limefuatiliwa kwa mawasiliano na nchi jirani. Kurejea kwa wasafiri wa Mashhad pia kunafuatiliwa. Alisema tuna jukumu la kulinda maisha ya raia na kuongeza: Tunajua kwamba maadui wahalifu hawataacha uhalifu wowote; bila shaka, safari za ndege zimekanseliwa hadi ilani nyingine. Mzigo wa usafirishaji wa abiria umeanguka kwenye sekta ya reli na barabara.

Tumechukua maamuzi makini katika hali ya vita pasina utani wowote 

Msemaji wa serikali alisisitiza: Tukiwa katika hali ya vita tumechukua maamuzi muhimu bila kutania kwa aina yoyote, na vita hivi viliwekwa juu yetu. Hatukuwahi kutaka vita na tulijaribu kuizuia. Licha ya kutoaminiana, tulijadiliana na tukawa tayari kuwasilisha programu yetu katika awamu ya sita, lakini hawakuacha nafasi kwa suala hili.

Aliongeza: "Kwa upande wa miundombinu, usafirishaji wa dawa, chakula na mafuta unaendelea kikamilifu na unasafirishaji unafanyika hadi miji yetu."

Mohajerani alisema: "Juhudi zinafanywa kuhakikisha kuwa hakuna abiria anayekwama mahali wanakokwenda. Juhudi zinafanyika kuhusiana na hili, na Waziri wa Shirika la Reli pia alihudhuria kwenye njia ya reli siku jana."

Alisema: "Pia, kufuatia shambulio kwenye ghala la mafuta la Shahr-e-Rey, Waziri wa Mafuta kwa sasa yuko njiani kurejea kutoka bohari hiyo, na kwa sasa anasimamia shughuli za kuzima moto."

Msemaji huyo wa serikali alisema: "Ningependa kushukuru vyama vyote na vyama vya wafanyakazi vya madereva na wasafirishaji wa lori ambao wanafanya kazi sana na hawakuzungumzia masuala yoyote ya vyama vya wafanyakazi kwa maana yoyote ya kweli wakati huu na kutoa msaada kamili kwa serikali."

Mohajerani alikumbusha: "Wizara ya Jihad ya Kilimo pia inatoa msaada wa chakula kwa uratibu na Wizara ya Barabara. Tuko katika hali ya vita na sote tunapaswa kusimamia suala hili kwa pamoja. Pia tunayo hatua muhimu katika uwanja wa mafuta na kazi inapangwa."

Misikiti na njia za chini ya ardhi kuwa wazi kwa umma saa 24 kwa siku kuanzia leo usiku

Alitangaza: "Usalama wa watu pia uko kwenye ajenda wakati wa mashambulizi, na kuanzia usiku wa leo, shule, misikiti, na njia za chini ya ardhi zitakuwa wazi kwa umma saa 24 kwa siku kuanzia usiku wa leo. Pia tumetarajia shule kuwa mahali salama mapema, na shule nyingi zinajulikana kama sehemu salama kwa watu kukimbilia."

Msemaji huyo wa serikali pia alibainisha kuwa vituo vinavyotoa huduma za moja kwa moja, kama vile benki na vituo vya matibabu, vinawahudumia wananchi. Vituo vingine vinatoa huduma kupitia mchanganyiko wa utumiaji simu na uwepo wa kimwili, kwa uratibu na wasimamizi husika.

Akiwahutubia wananchi wa Iran, Mohajerani alisema: "Shambulio la adui lilikuwa dhidi ya watu wa Iran, na wanasema uwongo, wakisema hatulengi maeneo ya makaazi. Unaona picha na kukumbuka kwamba walisema kitu kimoja kuhusu Lebanon, lakini ni mashambulizi ya kikatili yaliyoje waliyoyafanya kwenye maeneo mbalimbali ya makazi. Huu ni uvamizi wa wazi dhidi ya Iran, na ni lazima tusimame pamoja kwa ajili ya Iran; Wairan wote walio nje ya nchi na Wairan wote waliopo ndani ya nchi."

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha