Ali Larijani, katibu wa Baraza Kuu la Usalama la Taifa la Iran, amesema katika ujumbe kwenye X kwamba Tehran iko tayari kwa ajili ya mazungumzo na Washington, lakini mtindo wa Marekani unadhoofisha uwezekano wa mazungumzo ya maana. “Njia ya mazungumzo na Marekani haijafungwa; lakini ni Wamarekani ndio wanaotoa maneno tu bila kuyatekeleza, hawafiki kwenye meza ya mazungumzo, na wanailaumu Iran kwa hali hiyo,” Larijani ameandika.
“Kwa hakika, tunatilia mkazo mazungumzo yenye manufaa. Kwa kuibua masuala yasiyotekelezeka kama vile vikwazo vya makombora, wanachochea mazingira yanayozuia mazungumzo.”
Iran ilifanya duru tano za mazungumzo kuhusu kurejesha makubaliano ya nyuklia ya 2015 na wakati ikiwa imesalia siku mbili kabla ya duru mpya ya mazungumzo ikashambuliwa na utawala haramu wa Israel na Marekani yenyewe mwezi Juni.
Marekani na washirika wake wa Ulaya wamekuwa wakisisitiza mara kwa mara kwamba makubaliano yoyote ya baadaye yashughulikie si tu shughuli za nyuklia za Iran bali pia mpango wake wa makombora ya masafa marefu.
Tehran imekataa mara kwa mara ombi hilo, ikisisitiza kwamba uwezo wake wa kijeshi hauwezi kujadiliwa kwenye meza ya mazungumzo.
Nchi za Ulaya zilizoshiriki katika makubaliano ya 2015—Uingereza, Ufaransa, na Ujerumani—hivi karibuni zilikamilisha mchakato wa kurejesha vikwazo vya Umoja wa Mataifa hali inayozidisha ugumu wa diplomasia kwa ajili ya kutatua mvutano huu.
342/
Your Comment