6 Septemba 2025 - 18:56
Qaswida Adhimu ya Sheikh Eid Wambua Yamsifu Mtume Muhammad (s.a.w.w) kwa Mapenzi ya Dhati +Video

Nukuu kutoka Sheikh Eid: “Mtume (s.a.w.w) si kiongozi wa wakati wake tu, bali ni nuru inayomulika vizazi vyote. Qaswida hii ni wito wa upendo, ufuasi na kuhuisha sunna zake katika kila nyanja ya maisha yetu.”

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Katika kuadhimisha Maulidi ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) – Siku tukufu ya kuzaliwa kwa Mbora wa Viumbe, ambaye ni Rehma kwa walimwengu wote – Sheikh Eid Wambua, mmoja wa Wasomi wa Sayansi ya Dini na washairi mahiri wa mashairi ya Kiislamu, ameandaa Qaswida adhimu ya kumsifu Mtume Mtukufu (s.a.w.w).

Qaswida hii imejaa mapenzi ya kweli na ikhlasi kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) na Ahlul-Bayt wake (a.s), ikieleza kwa hisia, adabu na lugha ya juu ya maadili, utukufu, na nafasi ya kipekee ya Mtume katika maisha ya Waislamu na walimwengu wote.

Sheikh Eid Wambua, ambaye anatambulika kwa mashairi yenye misamiati mizuri, ujumbe wa kina na fikra za kuamsha mioyo, anasema kuwa Qaswida hii:

"Ni sadaka ya mapenzi ya dhati kwa Mtume (saww) na juhudi ya kumletea Ummah mwanga wa maadhimisho ya kuzaliwa kwa nuru ya uongofu, Muhammad al-Mustafa (s.a.w.w)."

Qaswida hiyo, ambayo imekuwa ikisambaa katika majukwaa ya Maulidi na mitandao ya kijamii, inaeleza visa vya maisha ya Mtume, huruma yake kwa Ummah, mapambano yake ya kuleta haki, na nafasi ya Ahlul-Bayt (a.s) katika kuendeleza ujumbe wake.

Mashairi hayo si tu ni burudani ya kiroho, bali pia ni njia ya kufundisha historia, maadili na mshikamano wa Kiislamu kupitia sanaa ya Kiswahili fasaha.

Nukuu kutoka Sheikh Eid:

“Mtume (s.a.w.w) si kiongozi wa wakati wake tu, bali ni nuru inayomulika vizazi vyote. Qaswida hii ni wito wa upendo, ufuasi na kuhuisha sunna zake katika kila nyanja ya maisha yetu.”

Tamasha la Qaswida hiyo linatarajiwa kufanyika kesho Jumapili Tarehe 07-09-2025,  katika hafla adhimu ya Maulidi ya Mtume Muhammad (saww) itakayofanyika Kigamboni katika Chuo cha Kidini cha Kidini cha Hazrat Zainab (sa), ambapo waumini wengi wamealikwa kusikiliza na kufaidika na ujumbe wake.

Your Comment

You are replying to: .
captcha