Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- tarehe 27 Septemba 2024 ilikuwa siku ngumu na chungu katika historia ya taifa la Lebanon. Katibu Mkuu wa Hizbullah, Shahidi Sayyid Hassan Nasrallah, aliuawa shahidi na utawala wa Kizayuni katika uwanja wa mapambano ya kulitetea taifa la Palestina lisilo na ulinzi na katika njia kubwa ya Quds.
Baadhi ya wafuasi na wapenda Nasrallah kwa muda mrefu hawakuweza kuamini kuwa kweli ameuawa shahidi. Kwao, Sayyid hakuwa tu kiongozi au katibu mkuu, bali alikuwa baba, mlezi, na mwalimu mwema aliyejitahidi maisha yake yote kuwaelimisha watu wa Lebanon, kulinda usalama wao na mipaka yao dhidi ya njama za Marekani, baadhi ya nchi za Kiarabu na utawala wa Kizayuni, bila kuruhusu hata shubiri ya ardhi ya Lebanon iingie mikononi mwa maadui.
Katika muktadha huu, Hidaya Sinan, mwongozaji wa maigizo ya televisheni na msimamizi wa shughuli za sanaa katika shule za al-Mustafa nchini Lebanon, alisimulia kumbukumbu zake kuhusu Shahidi Sayyid Hassan Nasrallah katika mahojiano maalum na mwandishi wa ABNA.
Kumbukumbu zake na Sayyid Nasrallah
Hidaya alisema:
“Nilikutana na Sayyid Nasrallah mara ya kwanza nikiwa bado katika umri mdogo wa taklifi. Tulimwomba ushauri, naye akatunasihi tuwe na subira ya juu, tumtendee wema mzazi wetu, na daima tusimame imara katika Hali".
Baada ya mwaka mmoja, nilipata tena fursa ya kukutana naye. Alitunasa ushauri kuhusu masuala ya maadili, kuswali kwa wakati, kushikamana na hijabu, na zaidi ya yote kuwa na mapenzi ya dhati kwa Wilayat al-Faqih. Kabla ya hapo tulikuwa tunampenda Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, lakini Sayyid Hassan ndiye aliyefanya mapenzi yetu kwa Wilayat al-Faqih yawe ya kina zaidi. Alitufundisha namna ya kuyeyuka katika uongozi huo.”
Alisimulia pia tukio ambapo alikuwa akihudumia idara ya sauti na spika katika hafla moja ya Sayyid. Ghafla umeme ukakatika na watu wakaanza kulalamika. Lakini Sayyid, kwa upole na tabasamu lake, aliwatuliza wananchi na kuwaomba wampatie nafasi Hidaya afanye kazi yake ipasavyo.
Katika tukio jingine la maigizo, mtoto mdogo alikuwa jukwaani akijaribu kufungua mlango ambao ulikuwa umekwama kwa sababu ya zulia lililokuwa nyuma yake. Wote hawakugundua, lakini Sayyid aliona mara moja na akaashiria suluhisho, jambo lililoonesha umakini wake wa ajabu.
Sifa za Kimaadili za Sayyid Nasrallah
Kwa mujibu wa Hidaya:
“Sayyid Hassan Nasrallah, pamoja na kuwa katika kilele cha maadili, alikuwa mnyenyekevu mno, mwenye huruma, na aliwapenda watu kwa dhati. Alikuwa kielelezo cha utu mwema. Hotuba zake zilikuwa zikigusa kila hitaji la jamii — kuanzia maadili, malezi, ndoa, mahusiano ya kijamii, hadi masuala mazito kama dawa za kulevya. Hakuna hoja ya kijamii aliyewahi kuacha kuizungumzia.”
Alisimulia pia kwamba walipokuwa wakijiandaa kuandaa tamthilia kuhusu Bibi Zaynab (a.s), walihitaji vyanzo vya rejea. Wakati huo huo walihudhuria moja ya hotuba za Sayyid. Ghafla akazungumzia moja kwa moja masuala yote waliokuwa wanayahitaji kwa ajili ya tamthilia yao — kana kwamba alikuwa anajua ni nini kilikuwa mioyoni mwao.
Hidaya alihitimisha:
"Kwetu sisi, Sayyid alikuwa ni Hazrat-e-Ishq - mfano wa Mapenzi safi. Alikuwa mwalimu na kiongozi wetu. Tunaomba kwa Mwenyezi Mungu kwamba tukipewa uhai na tukaona kudhihiri kwa Imam Mahdi (a.t.f.s), Sayyid Hassan pamoja na mashahidi wengine warejee, ili tuwe pamoja nao katika uwanja wa jihadi na mapambano ya haki. Inshallah.”
Your Comment