Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limetangaza wazi kwamba halitaacha kutoa msaada kwa wapiganaji wa Muqawamah na vikundi vyote vya Upinzani vinavyojitahidi kupigania uhuru wa nchi zao dhidi ya mababeru wa ukoloni na mashambulizi ya jinai ya Jina za Kizayuni.
Kauli hii imetolewa katika muktadha wa kuunga mkono harakati za mapambano za wananchi walioko kwenye hali ngumu za ukandamizaji na ukoloni katika ukanda wa Gaza, huku Iran ikiashiria dhamira yake ya kimkakati ya kuendeleza usaidizi wake wa kisiasa, kifikra na kijeshi kwa wale wanaopigania uhuru wa taifa lao.
Hatua hii ya Iran inaashiria msimamo wake thabiti katika kuhimiza uhuru na kuunga mkono harakati za kupinga ukandamizaji wa kigeni na ukoloni duniani kote.
Your Comment