Levinson ameandika kuwa, hadi siku ya mwisho ya vita, harakati hiyo ya ukombozi wa Palestina imeweza kuduumisha muundo wake wa kitaasisi, uongozi wake wa kisiasa, kamandi ya kwenye medani ya vita na udhibiti wa Ukanda wa Ghaza.
Mwandishi huyo wa gazeti la Haaretz ameendelea kueleza kwamba, hakuna kiongozi yeyote wa Hamas aliyeasi na kujitoa kwenye harakati hiyo kwa kuanzisha harakati ya upinzani, kusalimu amri au kuwauza mateka kwa pesa.
Levinson anasisitiza kuwa, harakati ya Hamas imehitimisha vita ikiwa imeweza kupata mafanikio mawili makuu: kwanza ni kuweza kuifufua na kuirejesha kadhia ya Palestina kwenye ulingo wa kimataifa na pili ni kuweza kuwakomboa wafungwa wa Kipalestina.
Mbali na Chaim Levinson, Avi Yassahroff, mchambuzi wa masuala ya Kiarabu katika gazeti la Yedioth Ahronoth yeye amesema, Hamas imeishinda Israel katika ilivyoanzisha dhidi ya Ghaza katika ulingo wa kisiasa na kimataifa na akaongezea kwa kusema, uharibifu uliofanywa na jeshi la utawala huuo na idadi kubwa ya Wapalestina waliouliwa katika vita hivyo wengi wao wakiwa wanawake na watoto vitazidisha chuki dhidi ya Israel, si huko Ghaza tu bali duniani kote.../
Your Comment