5 Novemba 2025 - 14:37
Source: ABNA
Maandamano ya Siku ya Kupambana na Ubeberu yanaendelea hivi sasa kwenye miji 900 ya Iran

Maandamano ya Siku ya Mwenyezi Mwenyezi Mungu yaani Aban 13 ambayo ni Siku ya Taifa ya Iran ya Kupambana na ubeberu na uistikbari yanaendelea hivi sasa hapa mjini Tehran na katika zaidi ya miji 900 kote humu nchini.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Fars, Aban 13  ambayo ni kumbukumbu ya harakati ya wanafunzi wa Iran ya kuuteka ubalozi wa Marekani uliokuwepo Tehran  kutokana na ubalozi huo kufanya ujasusi mwanzoni mwa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya mwaka 1979 nchini Iran, yameanza saa tatu asubuhi kwa saa za hapa Tehran katika miji zaidi ya 900 kote nchini Iran. Kwa hapa Tehran, kituo cha kuanzisha maandamano hayo kimekuwa ni  Uwanja wa Palestina kuelekea Mtaa wa Taleghani kwenye pango la kijasusi yaani sehemu ulipokuwepo ubalozi wa Marekani hapa Tehran.

Kaulimbiu kuu ya maandamano hayo ni kupinga ubeberu na uistikbari hasa wa Marekani. Skuli 120,000 za Iran zimepiga kengele za kuadhimisha siku hii huku walimu wakuu na wakuu wa skuli zote wakishiriki kikamilifu katika maandamano ya leo ya wanafunzi kote nchini Iran.

Ili kurahisisha idadi kubwa ya wanafunzi kushiriki kwenye maandamano hayo, Manispaa ya jiji la Tehran imeongeza safari za matreni ya chini ya ardhi yaani metro na mabasi ya mwendo kasi ili kuwasaidia wanafunzi hao.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha