22 Desemba 2025 - 14:30
Source: ABNA
Baghaei: Makombora ni kwa ajili ya kulinda taifa na hayawezi kujadiliwa

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje amesema: "Uwezo wa kiulinzi wa nchi, ulioundwa ili kuwazuia wavamizi kutokana na wazo lolote la kuishambulia Iran, si suala linaloweza kujadiliwa."

Esmail Baghaei, katika mkutano wake na waandishi wa habari Jumatatu asubuhi, akigusia matukio ya kikanda, alisema: "Eneo letu bado linakabiliwa na tatizo la kudumu la kuendelea kwa jinai za utawala wa Kizayuni. Matukio ya Gaza yasitufanye tusahau kinachotokea katika Ukingo wa Magharibi."

Aliendelea kusema: "Mpango wa makombora wa Iran umeundwa kwa ajili ya kulinda mamlaka ya Iran. Hapa tunakabiliwa na unafiki wa wazi. Mpango wa ulinzi wa Iran unaonekana kama tishio, wakati silaha nyingi zinapelekwa kwa utawala wa Kizayuni. Vikosi vyetu vya ulinzi vinajua vizuri jinsi ya kujilinda, hivyo vitaendelea na majukumu yao bila kujali chokochoko hizi."

Your Comment

You are replying to: .
captcha