Kwa mujibu wa shirika la habari la ABNA, chanzo katika mahakama ya kifalme ya Saudia kimesisitiza kupitia televisheni ya Channel 12 ya Israel kuwa hatua ya utawala huo kuitambua Somaliland imeibua hasira ya Riyadh.
Chanzo hicho kiliongeza kuwa mchakato wa kurejesha uhusiano wa kawaida (normalization) kati ya Riyadh na Tel Aviv umekuwa mgumu zaidi. Kuitambua Somaliland kumesababisha njia ya kurejesha uhusiano kuwa mbali na kuongeza kutengwa kwa utawala huo katika eneo.
Alisema: "Tamaa ya Netanyahu ya kutaka awamu nyingine ya uwaziri mkuu inachochea mivutano ya kikanda. Anazua mvutano ndani ya Israel na eneo zima. Kulenga usalama wa taifa wa Misri na kusimama dhidi ya nchi zote za Kiarabu na Kiislamu – ikiwemo nchi zilizotia saini mikataba ya kuhalalisha uhusiano kama UAE, Bahrain, Morocco na Sudan – ni tishio la wazi. Sera za Tel Aviv zinalenga utulivu wa Somalia. Netanyahu, kama kawaida, amekiuka sheria za kimataifa. Atahisije ikiwa Saudi Arabia itaunga mkono harakati za ukombozi huko Palestina na Kusini mwa Lebanon? Je, ataona hatua hiyo kama tangazo la vita? Baada ya vitendo hivi, bado atazungumzia kuhalalisha uhusiano? Huu ni wazimu gani."
Your Comment