Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Yair Lapid, kiongozi wa upinzani wa utawala wa Kizayuni, ametoa wito kwa serikali ya United States kuitangaza Qatar kuwa “nchi adui”.
Lapid aliyasema hayo katika mkutano wa “Conference of Presidents of Major American Jewish Organizations”, akidai kuwa shughuli na uwekezaji wa kifedha wa Qatar katika vyuo vikuu vya Marekani umechangia kuenea kwa “chuki dhidi ya Wayahudi na Uislamu wa msimamo mkali”.
Aidha, alitangaza kuwa amewasilisha pendekezo katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu (Israeli), ambalo kwa mujibu wake linalenga kuitambua Qatar kisheria kama nchi adui. Katika sehemu ya hotuba yake, alidai: “Qatar ni adui wa Marekani, adui wa Israeli na adui wa dunia.”
Your Comment